Afisa
Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndg.Mohamed Kiula, akieleza
hali ya utekelezaji wa Kampeni ya Afya na usafi wa mazingira katika
wilaya ya Kishapu kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally
N.Rufunga mapema wiki hii alipofanya ziara wilayani hapo katika kijiji
cha Bupigi kata ya Uchunga,kukagua utekelezaji wa kampeni hiyo ikiwa ni
maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya
Kikwete kuhamasisha jamii kubadili tabia na mtazamo wa jamii katika
kutathmini suala la usafi wa mazingira.
Wananchi
wa kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga wilaya ya Kishapu wakifanya zoezi
la uchefuaji kwa kuongozwa na Afisa Afya wa Halmashauri hiyo ili
kuwahamaisha kubadili tabia ya kujisaidia vichakani hali inayosababisha
uchafuzi wa mazingira na hivyo kupata magonjwa ya milipuko kama
kuharisha, kipindupindu na matumbo.
Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa Ally N. Rufunga akiwaeleza umuhimu wa kutunza mazingira
wananchi wa kijiji cha Bupigi wilaya ya Kishapu mapema wiki hii
alipotembelea kijijini hapo kuona utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya
Afya na usafi wa mazingira.
Baadhi
ya wananchi katika kijiji cha Nyamilangano wilaya ya Kahama
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga(hayupo pichani),akiwaeleza
umuhimu wa vyoo na usafi wa mazingira.
Katika
ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyofanya kwenye Halmashauri ya
wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Mji Kahama pamoja na Halmashauri ya
wilaya ya Ushetu ametoa rai kwa wananchi kutizama upya suala la mila na
desturi kwa baadhi ya makabila kutotumia choo kimoja na wakwe
linasababisha uchafuzi wa mazingira kwani inabidi wakati fulani wakwe
kujisaidia vichakani pale wanapotembelewa na wakwe zao. Hivyo amewataka
wananchi kuacha mila hizo kwani hakuna madhara yoyote,vinginevyo kaya
hizo ziwe na vyoo viwili.
Amewataka
pia viongozi hasa Wakuu wa wilaya kusimamia sheria ya uchafu wa
mazingira inayomfunga mtu yeyote mwenye kosa hilo kwa mwaka mmoja au
faini ya Tsh.Milioni moja.
Mkuu
wa Mkoa ametembelea vijiji vya Bupigi wilaya ya Kishapu, Mpunze
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Nyamilangano katika Halmashauri ya
Mji Kahama ili kuona hali ya utekelezaji wa kampeni hiyo.
Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga
0 comments:
Post a Comment