Home » » DC Kahama ataka kusitishwa kwa michango ya maendeleo wakati wa kilimo

DC Kahama ataka kusitishwa kwa michango ya maendeleo wakati wa kilimo

MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya amewataka madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhakikisha watendaji wao ngazi ya Kata wanasimamisha michango ya Maendeleo wakati wa msimu wa Kilimo.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akifungua kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo amedai michango mwisho mwezi wa kumi ili kuwapa fursa wananchi kujiandaa na kilimo.

Ameonya kuwa watendaji watakaochangisha wakati wa kilimo atawachukulia hatua kali kwakuwa hataki wananchi wasumbuliwe wakati wa kilimo ambapo katika wilaya ya Kahama ameweka msimamo huo.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Machibya Jiduramabambasi amesema kikao cha baraza hilo kimejadiri mambo mbalimbali ikiwemo kuundwa kwa tarafa tatu katika halmashauri hiyo,za Zongomera,Kahama mjini na Isagehe.

Wilaya ya Kahama imegawanywa kwenye Halmashauri tatu za Mji,Ushetu na Msalala ambapo kila Halmashauri imeanza mikakati ya kuboresha maeneo ya kiutawala zikiwemo tarafa ,kata na Vijiji.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa