Home » » Madiwani wakerwa Lembeli kutumia fedha za mfuko wa jimbo

Madiwani wakerwa Lembeli kutumia fedha za mfuko wa jimbo

MVUTANO mkubwa umeibuka katika Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wa kupinga maazimio ya kumuita kwenye Kikao Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli ili atoe maelezo juu ya matumizi ya fedha ya Mfuko wa Jimbo.

Hoja ya kumuita Mbunge huyo iliibuliwa jana kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji ambapo Diwani wa Kata ya Busoka, Mussa Mabubu kuhoji uhalali wa fedha hizo kutumiwa na Mbunge huyo bila kuwashirikisha madiwani.

Hata hivyo hoja hiyo ilifafanuliwa na Afisa Mipango wa Mji wa Kahama, Jordan Ojode ambaye amedai fedha hizo hutolewa na serikali kwa ajili ya kusaidia nguvu za wananchi kwenye shughuli za maendeleo.

Bwana Ojode amesema baada ya kufikishwa kwenye Halmashauri hutumiwa kwenye majimbo na muhusika akiwa ni Mbunge wakati akitembelea wananchi na kukuta wameanza mradi huzitumia kusaidia nguvu hizo.

Pamoja na maazimio hayo ya kumuita Mbunge huyu ili a toe maelezo juu ya fedha hizo tayari Madiwani hao wamegawanyika huku idadi kubwa wakipinga kuitwa kwa madai tayari mfuko huo umewasaidia katika shughuli za maendeleo ya wananchi wao

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa