WAKULIMA wa tumbaku
wilayani Kahama ‘Kitumbaku Mkoa’ wameendelea kumwangukia Rais Jakaya Kikwete
kutosaini sheria ya ushirika 2013 yenye lengo la kukifuta Chama Kilele (Apex)
cha wakulima wa zao hilo nchini, kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuwatia
ufukara.
Mkulima, Shija
Malambo wa Kijiji cha Bulungwa na Maliseli Kazimoto wa Bulowa, kwa nyakati
tofauti walimsihii Rais Kikwete kutosaini sheria hiyo na kumuomba akutane nao.
Walisema kuwa endapo
rais atasaini na kuifuta Apex, zao hilo litakufa kama ilivyo kwa kahawa, pamba
na korosho.
“Kahawa na pamba
yakiwa na Apex zao yalikuwa kinara kuliingizia taifa fedha za kigeni, serikali
ilipozifuta Apex, mazao yamekuwa mzigo kwa mkulima na serikali na mapato yake
yameshuka maradufu, tunamuomba Rais Kikwete aendeleze busara zake kama
alivyofanya kwenye suala la Katiba atuokoe walalahoi,” alisema Kazimoto.
Wakionesha
kushangazwa na wabunge na serikali kung’ang’ania Apex ifutwe, wakulima hao
walimkumbusha Rais Kikwete kuwa mbali na vyama vyao ikiwemo Apex kuwapo
kisheria pia ni vyama vya hiari vilivyowekwa na wakulima kuwaongezea nguvu ya
utetezi wa matatizo na changamoto za uzalishaji na masoko.
Walisema
walishangazwa na Waziri Christopher Chiza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku
nchini, Wilfred Mushi, kuwa Apex ni ya wahuni wenye nia ya kuwaibia wakulima na
kumuomba rais awaite na kuwauliza vizuri, vinginevyo wawajibishwe kwa
uchochezi.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika ‘Mkoa wa
Kahama’ Kitumbaku KACU Ltd, Emanuel Peter, alisema mbali na wakulima kuwa
na madai hayo tayari imeundwa kamati ya kuonana na rais juu ya jambo hilo
ambayo inakwamishwa na watendaji wake wa karibu
0 comments:
Post a Comment