Home » » WANAOKATA MAPANGA VIKONGWE KUNYONGWA

WANAOKATA MAPANGA VIKONGWE KUNYONGWA

Wakazi wa Lulembela Wilaya ya Bukombe Joseph Lushika na Maziku Mpikachai, watanyongwa mpaka kufa kwa kupatikana na hatia ya kumwua kwa kumkatakata mapanga Monica Bulemela nyumbani kwake Machi 6, 2005 saa 3:00 usiku.

Adhabu hiyo imetolewa na Jaji Simon Lukelelwa katika kikao cha Mahakama kuu Kanda ya Tabora kinachoendelea mjini Shinyanga kusikiliza kesi za mauaji.

Mapema upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa serikali Onesmo Lwenge, umedai kuwa washitakiwa kwa  pamoja walivamia mji wa marehemu saa hizo wakati marehemu na familia yake wakiwa nje wakipata chakula cha usiku.

Walimkatakata kwa mapanga marehemu sehemu za paji la uso, shingoni na bega la kushoto na sehemu zingine za mwili hadi kufa.

Akitoa adhabu hiyo, Jaji Lukelelwa, amesema Mahakama imeridhika na ushahdi ulitolewa na upande wa mashtaka ambao umethibitisha kosa pasipo kuacha mashaka yoyote dhidi ya washitakiwa wote wawili.

Jaji Lukelelwa amesema, adhabu pekee kwa mtu anayepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia mmpaka sasa ni kifo, washitakiwa wote wawili watanyongwa mpaka kufa.

Washitakiwa wanayo haki ya kuomba rufaa ndani ysiku 30

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa