Home »
» CHADEMA YAANZA MIKAKATI 2015
CHADEMA YAANZA MIKAKATI 2015
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amewataka watendaji wa chama
hicho nchi nzima, kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa 2014, Uchaguzi Mkuu 2015.
Bw. Mbowe aliyasema hayo Mjini
Kahama, mkoani Shinyanga, mwishoni mwa wiki akiwa katika ziara ya
kichama Kanda ya Ziwa Mashariki, inayojumuisha Mikoa ya Mara, Simiyu na
Shinyanga.
Ziara hiyo imeanza Novemba Mosi mwaka huu, ambapo Bw.
Mbowe alikutana na Baraza la Mashauriano la mkoani humo na kukagua uhai
wa chama katika kanda hiyo.
Pia Bw. Mbowe alikutana na wadau wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki na kupanga mikakati ya kuimarisha kanda hiyo.
Novemba
2 mwaka huu, alikutana na Baraza la Mashauriano mkoani Mara na kuwataka
viongozi pamoja na wanachama wa Mkoa huo, kuweka mikakati ya kuimarisha
hadhi ya chama ili kufanikisha harakati za ukombozi wa nchi na
kupigania mabadiliko kama inavyokuwa siku zote.
Ofisa Mwandamizi wa
Habari CHADEMA Makao Makuu, Bw. Tumaini Makene, alisema kwa kauli moja,
viongozi wa Baraza la Mashauriano Mkoa wa Mara, waliazimia kuanza
'Operesheni Imarisha CHADEMA Mara', ambayo itazinduliwa hivi karibuni na
kufanyika Mkoa mzima.
Alisema kupitia uongozi wa kanda wenye
mamlaka ya kusimamia na kuimarisha chama katika mikoa yote husika, Bw.
Mbowe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali kila mmoja kwa nafasi yake
kutimiza wajibu wa kukifanya CHADEMA kiendeleekuwa sauti ya Watanzania
wote, wanaosaka haki nchini.
Aliwataka wawe viongozi kwa maneno na
vitendo akisisitiza umuhimu wao wa kuwa taswira chanya mbele ya jamii
pamoja na kukiwakilisha chama kwa kuzingatia uadilifu, uwezo na
uwajibikaji kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania ambao chama hicho
kinataka kuwaongoza.
Bw. Mbowe alisisitiza umuhimu wa vikao vya
kikatiba, mafunzo na mikutano ya wanachama katika usimamizi, uendeshaji
wa chama hasa wakati huu ambao Watanzania wameweka matumaini ya kufanya
mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kupitia CHADEMA
CHANZO;MAJIRA
0 comments:
Post a Comment