ZAIDI
ya watoto 78 waishio katika mazingira Hatarishi katika kijiji cha
Nduku Kata ya Kinaga Wilayani Kahama Wamepatiwa msaada wa vifaa
mbalimbali pamoja na nguo za shule, kalamu, daftari, mafuta ya kupakaa, godoro
pamoja na shuka vikiwa na thamani ya sh. Laki tano.
Hali
hiyo imeelezwa jana na Katibu msaidizi wa kikundi cha Tumaini centre;
Nzile Lukondya, katika hafra fupi ya kugawa misada hiyo iliyofanyika
katika kijiji cha Nduku wilayani Kahama.
Akikabidhi
misaada hiyo Diwani wa kata ya Kinaga bi.Mary Manyambo aliwataka viongozi
wa kikundi hicho kuhakikisha wanafanikiwa katika hatua hiyo ya kuwasaidia
watoto wa mitaani hali ambayo itapunguza mzigo kwa serikali pamoja na wimbi la
watoto wa mitaani.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kikundi hicho ;Mussa Mayala ameeleza mikakati iliyopo
ni kuhakikisha kinalenga kuwasaidia vijana,wanawake na wanaume ili waweze
kujipatia maisha yao wenyewe kwa kujitegemea pia waweze kuthanminika kaitika
jamii inayowazunguka pamoja na kupata ofisi maalum.
Mmoja
wa wazee wasiojiweza; Mathias Luhenzagula ambae pia ni mlemavu wa macho
aliushukuru uongozi wa kikundi hicho kwa kumpatia msaada wa godoro na shuka,
kutokana nakuwa tangu azaliwe hajawahi kulalia godoro ambapo sasa atakuwa
amelipatia ukubwani .
0 comments:
Post a Comment