JIBU LA SWALI LA MBUNGE Meatu
SERIKALI imetoa jumla ya sh bilioni 2.09 kwa vikundi mbalimbali vipatavyo 827 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Hayo yalielezwa bungeni mjini hapa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa
Ghasia, wakati alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Meatu,
Jeremiah Opulukwa (CHADEMA).
Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua ni fedha kiasi gani
zimekwisha kutolewa kwa vikundi mbalimbali katika Wilaya ya Meatu hadi
sasa. Akiendelea kujibu swali hilo, waziri huyo alisema kuanzia mwaka
1996 hadi kufikia Juni, 2013 jumla ya sh milioni 78.6 zimetolewa kwa
vikundi vipatavyo 172, ikiwa ni mkopo wenye marejesho.
“Kati ya fedha hizo sh milioni 29.9 ni kutoka katika Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu, sh milioni 10 kutoka Wizara ya Kazi na Maendeleo ya
Vijana, sh milioni 39 ni kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto,” alisema.
Aidha, alisema Ghasia jumla ya sh milioni 84.3 zimetolewa kwa vikundi
76 kutoka katika fedha za mfuko wa jimbo na kuongeza kuwa jumla ya
fedha kiasi cha sh bilioni 1.9 zimetolewa kwa vikundi 579, ukiwa kama
msaada kupitia Programu ya Maendeleo ya Mazingira ya Ziwa Victoria
Awamu ya Pili (LVEMP II) sh milioni 192, TASAF sh milioni 656 na Mfuko
wa Maendeleo ya Wanawake.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/14 Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu imepanga kutoa mikopo kiasi cha sh milioni 153 kwa
vikundi mbalimbali vikiwamo vikundi vya wanawake sh milioni 50,
vikundi vya vijana sh milioni 50 na vikundi vya watu waishio na VVU sh
milioni 53.
Alifafanua kuwa kati ya fedha hizo sh milioni 100 ni kutoka katika
bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na sh milioni 53 ni kutoka kwa
washirika wa maendeleo.
chanzo;tanzania daima
0 comments:
Post a Comment