Mkurugenzi wa Kiwanda cha "Triple S" ndg.Salum Self akimweleza Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga(hayupo pichani) matarajio ya kufungua kiwanda hicho
cha nyama jana alipotembelea kiwandani hapo.Picha na Magdalena Nkulu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha nyama cha "Triple S" (hayupo pichani) wakati alipotembelea kiwanda hicho jana.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bi.Honorata Ruhumbika.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha nyama cha "Triple S" (hayupo pichani) wakati alipotembelea kiwanda hicho jana.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bi.Honorata Ruhumbika.
Picha ya pamoja na Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga na Mkurugenzi wa kiwanda,na wataalam
wengine wa Mkoa na Manispaa alipotembelea kiwanda cha nyama cha "Triple S" kilichoko Manispaa ya Shinyanga jana.
***************************
Kiwanda cha kuchinja na kusindika nyama kilichopo Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga,kinatarajiwa kufunguliwa wakati wowote baada taratibu za mwisho za makubaliano na
wafanyabiashara wa ng'ombe na mbuzi kukamilika.
Mkurugenzi
wa Kiwanda hicho cha 'Triple S' ndugu Salum Self amesema majaribio
yameshafanyika,na wako katika hatua ya mikataba ya awali na
wafanyabiashara hivyo wananchi
wategemee wakati wowote kiwanda kitaanza kazi ya kusindika nyama.
Ndugu
Salum amesema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally
N.Rufunga jana, aliyetembelea kiwanda hicho ili kujua kimefikia hatua
gani ya utekelezaji.
Kiwanda
hicho kilichojengwa na serikali miaka 35 iliyopita na baadaye kuuzwa
kwa mwekezaji huyo, kitafunguliwa na kiongozi wa kitaifa na kinatarajiwa
kuchinja ng'ombe 300 na mbuzi 2000 kwa siku.
Aidha,Ndg.
Salum amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa, kiwanda kitaajiri zaidi ya
wananchi150 hivyo wananchi wa mkoa wa Shinyanga watanufaika pia katika
upande wa ajira, na zadi kiwanda kitaangalia pia wataalamu wa ndani ya
nchi kutoka chuo cha ufundi VETA.
Serikali
mkoani Shinyanga kwa kuongozwa na Mhe.Mkuu wa Mkoa Ally N.Rufunga,
imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhimiza uwekezaji katika viwanda
mbalimbali ili kuinua uchumi kwa kutumia fursa zinazopatika mkoani hapa
kama wingi wa mifugo,mazao ya chakula na biashara na madini.
Kiwanda hicho cha nyama ni moja ya juhudi hizo, kwani itakuwa ni mara ya kwanza kufanya kazi tangu kijengwe miaka ya 1970.
Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga
0 comments:
Post a Comment