Halmashauri
ya mji wa kahama mkoani shinyanga isaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya
lami baina yake na kampuni ya ujenzi ya Chico kutoka Nchini China.
Mkataba
huo ulisainiwa mbele ya Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya ambapo barabara
hiyo ya kiwango cha rami itakuwa na urefu wa kilometa 5.67 ambayo hadi
kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi billion 4.5 zakitanzania.
Mkuu
wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amesema Fedha hizo zimepatikana toka sahemu
mabalimbali ikiwemo kwa wawekezaji wa kampuni ya African Barrick Gold
Mine Buzwagi ambao walitoa kiasi cha shilingi 375,000,000 pamoja na fedha
iliyotolewa na Ofisi ya waziri mkuu kiasi cha shilingi million 700.
Mpesya
amesema ujenzi huo utaanza mara moja ambapo utamalizika ndani ya miezi sita na
kuongeza kuwa lengo kubwa ni kubadilisha mji wa kahama na kuufanya uwe na
mpangilio hali ambayo itafanya mji huo kuvutia na wenye mazingira safi .
Kwa
upande wake Afisa mahusiano toka katika mgodi wa Buzwagi David Kilala
amesema wataendelea kushirikiana na wananchi wa kahama kwa kuanzia
wameanza na barabara na wataendelea katika kuhakikisha wananchi
wananufaika na mwekezaji ananufaika ili kahama iweze kupiga hatua.
0 comments:
Post a Comment