Home » » Sekta ya viwanda Shinyanga kuajiri watu 30,000 ndani ya mwaka mmoja

Sekta ya viwanda Shinyanga kuajiri watu 30,000 ndani ya mwaka mmoja



Zaidi wa watu 30,000 watapata ajira katika sekta ya viwanda mkoani shinyanga kuanzia mwezi desemba 2013 hadi desemba 2014 kutokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda unaoendelea mkoani Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga bw Ally Nassoro Rufunga amesema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha Mussoma Food kilichopo manspaa ya Shinyanga,

Mkuu huyo wa mkoa amesema Shinyanga imegeuka kuwa mkoa wa viwanda na kwamba tayari viwanda vya soda na maji vya kampuni ya jambo vimefunguliwa.

Amesema mwezi januari viwanda vya nyama na ngozi vya wachina vitafunguliwa sanjali na kiwanda cha nguo pia cha wachina.

Bw Rufunga amesema kiwanda cha nyama cha Shinyanga ambacho kilijengwa na kukamiliaka miaka zaidi ya 20 na kushindwa kuanza kazi nacho kitafunguliwa mwezi januari.

Amesema hadi kufikia desemba 2014 zaidi ya viwanda 10 vitakuwa vimefunguliwa na kutoa fursa za kiuchumi kwa wafugaji na wakulima wa zao la pamba kupata bei za uhakika za mazao yao.

katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga ameupongeza uongozi wa kiwanda cha Mussoma Food kwa uwekezaji wake mkubwa mkoani shinyanga.

Awali mkurugenzi wa kiwanda hichi bw Said Magilagi amesema kwamba kiwanda chake kinatoa bidhaa bora za unga na mchele na kuiyomba serikali kuwaboreshea mazingira ya uwekezaji kwa wazawa

Hata hivyo mkurugenzi huyo alikabidhi tani 1 ya  unga kwa ajili ya kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi albino kilichopo manspaa ya Shinyanga

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa