JUMLA
ya wasichana 60 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 waliojifungua na
wengine kupata mimba wakiwa mashuleni Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
wameanza kupatiwa mafunzo ya Afya ya uzazi hali itakayowafanya kupata
elimu ya kujikinga na mimba za utotoni .
Katika mafunzo hayo yanayofanywa na shirika la Kiota Women Health and
Development wasichana hao wametoka katika kata Nne za Shilela
Lunguya,Busoka na Mhongolo baada ya kumaliza mafunzo hayo watapatiwa
elimu kwa mfumo usio rasmi kama vile MMEMKWA kwa wale wa shule za
msingi .
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka shirika hilo Emmanueli Yohana amesema kwa
wale waliokatisha masomo ya sekondari watapatiwa elimu hiyo kwa mfumo
wa QT pamoja na vyuo vya ufundi hali ambayo itawakwamua katika maisha
yao .
Hata hivyo Yohana amesema tayari wanafunzi hao wamepewa fomu za kujaza
ili kushiriki mafunzo hayo ingawa idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na
idadi kubwa zaidi ya wasichana chini ya umri huo waliokatisha masomo yao
kwa kupata ujauzito wakiwa shuleni.
Nae Mkurugenzi wa shirika hilo Justa Mwaituka amesema kuwa mradi huo ni
wa miaka miwili ambao utasaidia wasichana hao kujiepusha na umasikini
kwa kuwa tayari watakuwa wamejifunza stadi za maisha na kutoa elimu ya
madhara ya mimba za utotoni kwa wenzao walioko mashuleni.
Kwa upande wake mganga mkuu wa Halmashauri ya Msalala wilayani kahama
Hamad Nyambea amewaonya vikali wazazi kwa kitendo cha kuto chukua
hatua kwa wanaume wanaowapa mimba watoto hao .
Home »
» WALIOBEBA MIMBA WAKIWA NA UMRI MDOGO WAPEWA MAFUNZO YA AFYA NA UZAZI
0 comments:
Post a Comment