Home »
» MCHIMBAJI MADINI SHINYANGA ACHOMWA KISU,AFA
MCHIMBAJI MADINI SHINYANGA ACHOMWA KISU,AFA
Mchimbaji
mdogo wa madini ya dhahabu mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya
kuchomwa kisu kifuani katika ugomvi wa ku gombea mwanamke uliozuka kati
yake na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Cosmas Mazigo (23), mkazi wa
Misungwi mkoani Mwanza, anaripoti Suleiman Abeid, Shinyanga.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Evarist Ma ngala, amemtaja marehemu kuwa ni
Emmanuel Chacha (29), mkazi wa Kijiji cha Nyanga lata, wilayani Kahama
ambaye alifariki papo hapo ambapo tukio hilo limetokea juzi saa tano
usiku katika Kijiji cha Kalole, Kata ya Lunguya, wilayani Kahama.
Alisema
chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kugombea mwanamke ambaye jina lake
halikufa hamika mara moja ambapo wakati ugomvi huo ukiendelea, mtuhumiwa
alichukua kisu na kumchoma nacho Chacha kifuani.
Aliongeza kuwa,
baada ya tukio hilo wanakijiji waliokuwa jirani walifanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo ambaye hivi sasa anashikiliwa polisi na baada ya
upelelezi kukamilika, atafikishwa mahakamani kujibu shtakala mauaji.
Chanzo:majira
0 comments:
Post a Comment