Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea.
 Mkuu
 wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda 
hicho mapema leo alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea
 Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo
 Mkuu
 wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa 
matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k
 Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga
 Mkuu
 wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika
 kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho
 Ndani
 ya kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong ambapo Mkuu wa mkoa wa 
Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amekitembelea mapema leo na kujionea kazi 
ya kujaribu mitambo
=========  =========   ===========
Kiwanda
 cha kutengeneza Ngozi kwa ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya 
Kichina "Xiu hua"  kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani 
Shinyanga kimekamilika ambapo mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho 
"Mr.Way" amesema kwa sasa majaribio yanafanyika kabla ya kuanza 
uzalishaji wakati wowote.
Mkuu 
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho mapema
 leo na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za 
mbuzi,kondoo na ng'ombe.
Kiwanda
 hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi 
Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng'ombe 2500, kitaajiri zaidi ya 
Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa 
mkoa wa Shinyanga.
Mkuu 
wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong 
Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q 
kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza 
kazi ya uzalishaji. 
Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.
Aidha,kiwanda
 cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho  kinatarajiwa kuanza 
kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine 
mwishoni mwa mwezi Februari.
Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.
Mhe.Rufunga
 amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo 
vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura
 ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani 
amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga 
yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha 
ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.
MICHUZI BLOG 
 







 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment