MBUNGE wa Msalala wilayani Kahama, Ezekeil Maige, juzi aliingia
kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Ubagwe, Kahama na kumnadi
mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamis Majogolo.
Maige aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Lembeli ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ni
mahasimu wakubwa kisiasa licha ya wote kutoka wilaya moja ya Kahama.
Waziri huyo wa zamani, anamshutumu Lembeli kwa kuandika ripoti yenye
upotoshwaji mwaka 2012 na kumfanya aondolewe katika nafasi yake ya
uwaziri.
Kwa sababu hiyo, kitendo cha Maige kufika kwenye jimbo la hasimu wake
na kufanya kampeni hizo, kiliwashangaza baadhi ya wafuasi wa CCM kwa
kuwa ni mara ya kwanza tangu alipoondolewa kwenye uwaziri kufika Kahama
kwa shughuli za kisiasa.
Katika kampeni hizo, Maige alimuuunga mkono Lembeli kwa juhudi zake
za kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo na kuwashauri wakazi wa Ubagwe
wamchague Majogolo ili ashirikiane na mbunge wao kuharakisha maendeleo
kauli iliyozungumzwa pia na Lembeli kwa nyakati tofauti.
Uchaguzi mdogo utafanyika Februari 9 baada ya aliyekuwa Diwani wa Ubagwe, Robert Mdula kufariki dunia mwaka jana.
Vyama vingine vinavyoshiriki na wagombea wao kwenye mabano ni CHADEMA (Adam Ngoma) na Tadea (Machibya Lubinza).
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment