Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADHI ya wakazi wa mjini hapa wamepigwa na butwaa kuwaona baadhi
ya maofisa wa polisi wakitembeza bakuli mitaani wakiomba mchango wa
fedha kwa ajili ya ukarabati wa magari mabovu ya polisi.
Mshangao wa wakazi hao unatokana na zoezi linalodaiwa kufanywa na
baadhi ya maofisa wa polisi, wanaowatembelea wafanyabiashara mbalimbali
mjini hapa wakichangisha fedha wakidai zitasaidia kufanyia matengenezo
ya magari mengi ya polisi ambayo ni mabovu kwa kipindi kirefu.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, baadhi ya
wananchi walioshuhudia kuchangishwa kwa michango hiyo, walielezea
kutoamini walichokiona kwa vile si kawaida kwa taasisi za serikali
kutembeza bakuli kuomba michango ya fedha kwa ajili ya kuendeshea
shughuli zake za kila siku.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment