Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUENDESHA biashara bila ya kufuata misingi ya sheria, taratibu na maadili ni moja kati ya changamoto zinazowakabili wafanyabiashara mkoani Shinyanga kupata fursa ya kufanya biashara na Migodi ya Barrick Tanzania.
Hayo yalisemwa juzi na ofisa kutoka katika kitengo cha Ugavi katika Migodi ya African Barrick Gold, Dickson Liwumba katika kikao kilichowajumuisha wafanyabiashara waliopo mkoani Shinyanga na wale wanaofanya kazi na migodi hiyo kutoka sehemu mbalimbali Kanda ya Ziwa.
Liwumba alisema kuwa mbali na changamoto hiyo pia wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga wamekuwa hawapati fursa hizo pia kutokana na bidhaa zao kutokuwa na kiwango na kutomudu idadi ya vitu vinavyohitajika kwa wawekezaji hao.
Ofisa huyo alisema kuwa pia ushirikiano baina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga na kutoridhika pia katika suala zima la kujiendeleza nalo ni tatizo kubwa hatua ambayo inakuwa vigumu hata kuomba zabuni katika makampuni hayo pindi zinapotokea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua mkutano huo uliandaliwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine alisema kuwa wafanyabiashara hasa wa Mkoa wa Shinyanga wanapaswa kujua kuwa bado wana fursa kubwa ya kufanya kazi na migodi hiyo miwili.
Aliushukuru uongozi wa migodi hiyo miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kufanya mkutano na kutoa elimu kwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa Shinyanga katika kufuata sheria na muda katika kuendesha biashara zao hasa katika maeneo ya wawekezaji wa migodi.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment