Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VIONGOZI wa vyama vya siasa wanaotangaza nia ya kuwania urais katika
uchaguzi wa mwaka 2015 wametakiwa kupima uwezo wao wa kukabiliana na
matatizo ya jamii.
Matatizo hayo ni uporaji wa rasilimali, ufisadi, rushwa na mauaji ya albino kabla ya kujitangaza mbele ya wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa Shinyanga Mjini jana na Askofu William
Mwamalanga alipofungua Kongamano la Uelewa na Uzalendo kwa vijana 1,400
kutoka vyuo vya madhebu ya dini na kusema viongozi wasio na maadili,
uzalendo wenye kiburi na waliokosa usikivu ni chanzo cha mfarakano.
Mchungaji Mwamalanga alisema watu wanaoitaka ikulu mwakani
wasitegemee fedha walizo nazo kuwa kigezo cha kuingia huko bali wapime
misuli yao endapo inaweza kupambana na kero zinazolitesa taifa.
Shekhe Massoud Amiri Masoud, amekiri kuwa serikali ya awamu ya nne
imeshindwa kuwachukulia hatua vigogo wa dawa za kulevya licha ya kupewa
orodha ya majina yao mwaka 2006 lakini hakuna aliyekamatwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment