MGOMBEA Uenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nheleghani, Manispaa ya
Shinyanga, Deus Seni (CHADEMA) ameahidi kulinda raslimali za kijiji kwa
kuwabana wawekezaji.
Akijinadi katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo eneo la Madukani
kijijini hapo jana, Seni alisema atahakikisha anawabana wawekezaji wote
ili waheshimu na kutekeleza mikataba yao kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Aliwataka wananchi kumuunga mkono na kupuuza propagada za Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambazo ni kuwahadaa wananchi kwenye ardhi yao na
demokrasia.
Alisema utekelezaji wa sera ya uwekezaji ni nzuri, lakini uongozi na
serikali ya CCM inawajali zaidi wawekezaji wa nje kuliko wananchi wake
wanaopaswa kunufaika na raslimali zilizopo.
Alisema wawekezaji kutoka China wamejenga viwanda vya kusindika
mafuta ya pamba, alzeti na kusokota nyuzi za pamba licha ya kuketi nao
na kuahidi kutengeza madawati 300 kwa shule ya msingi ya Nheleghani,
kujenga magati ya maji kila kitongoji hadi sasa ahadi hiyo
haijatekelezwa huku akidai ni uzembe wa viongozi wa CCM kufuatilia.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment