Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza
kutolewa kwa umeme bure kwenye Kituo cha Ushirika wa Kutokomeza
Ukeketaji kilichopo Kata ya Gorong’a, wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Kituo hicho hutoa elimu kwa wasichana kuhusu kupinga mila ya ukeketaji.
Waziri Muhongo alisema hayo alipotembelea kituoni hapo na vijiji mbalimbali kukagua mradi wa umeme vijijini.
Profesa Muhongo alisema kituo hicho hakitalipa
gharama zozote za kuvutiwa umeme na kwamba Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) litawapa umeme bure ili uwasaidie kupata mwanga katika
shughuli zao mafunzo.
“Nawashukuru kwa ubunifu wenu wa kuanzisha kituo
hiki ili kuwasaidia wasichana waepuke kukeketwa... Tanesco itawapa umeme
bure, nawaomba wasichana msome kwa bidii tena masomo ya sayansi na
elimu mliyoipata iwajenge,” alisema.
Katika risala yao, wasichana hao walisema wamefika
hapo kwa ridhaa ya wazazi wao, lakini wapo wasichana waliokimbia
majumbani kukwepa kukeketwa.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Sista Baibika alisema
kuwa watu wapatao 634 kutoka Tarime na Serengeti wanaendelea na mafunzo
hayo yaliyoanza Desemba 10 na yatahitimishwa Januari 5 mwakani.
Alisema elimu hiyo hutolewa kila mwaka katika kipindi hiki cha ukeketaji mkoani Tarime
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment