Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser
Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu aliyekwenda kumuaaga ofisini kwake baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkugugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo alipokwenda kumuaga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga.
Meneja Miradi wa Shirika la AGPAHI Mkoa wa Shinyanga, Dk. Dk. Gastor Njau (kushoto) akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu akifafanua jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI alipokwenda kumuaga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akizungumza na uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI).
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akifafanua jambo wakati uongozi wa Shirika la AGPAHI ulipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Laurean Bwanakunu.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo
la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Ally Rufunga, wakati alipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya
kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akisoma cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu wakati alipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la AGPAHI. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Laurean Bwanakunu, Meneja Miradi wa Shirika hilo Mkoa wa Shinyanga, Dk. Dk. Gastor Njau na Mratibu wa Programu ya Mawasiliano na Huduma za Jamii, Jane Shuma.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga amesema
kasi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi mkoani hapa imepungua kutoka asilimia
9.1 mwaka 2011 hadi asilimia 4.9 mwaka 2014.
Rufunga alisema hayo ofisini kwake wakati
akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare
Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu ambaye ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) hivi karibuni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari,
Rufunga hakusita kupongeza juhudi za shirika hilo katika kuhakikisha
linapambana na maambukizi mapya ya VVU ili kufika kwenye ziro tatu.
“Wakati mnaingia Shinyanga mwaka 2011 kasi yetu
ilikua kubwa kuliko ile ya kitaifa na hadi kufika Juni,2015 tulifika asilimia
4.1 japo hili halijadhibitishwa na Wizara ya Afya ila tumeshafika huko,”
alisema mkuu huyo wa mkoa.
Alisema AGPAHI limejenga nyumba bora za kutolea
huduma za afya kwenye vituo vya afya na zahanati mbalimbali mkoani humo na
kuahidi kwamba ofisi yake itatenga bajeti ya kuzifanyia ukarabati na kuzitunza.
“Msd ndio uhai wetu hasa watanzani tunaoishi
vijijini, nakutakia kazi njema… waliokuteua hawakukosea, umefanyakazi nzuri kwa
kushirikiana na watumishi wengine wa AGPAHI.
“…Naamini utaendelea kuwa kiongozi bora hata
huko uendako, usiogope maneno maana kazi za utumishi wa umma lazima yawepo,”
alisema Rufunga huku akisisitiza kwamba wakazi wa Shinyanga wataendelea
kushirikiana na shirika hilo na kuenzi kazi wanazofanya.
Akimshukuru kwa ushirikiano, Bwanakunu alisema
kazi ya AGPAHI mkoani Shinyanga ilikua rahisi kwa kuwa alipata ushurikiano
kutoka kwa mkuu huyo wa mkoa na watumishi wengine wa idara ya afya.
“Naamini ushirikiano nilioupata kwako utaendelea
hata kwa atakayerithi nafasi yangu, tulipoanza Shinyanga ilikua katika hali
mbaya ya maambukizi lakini sasa tunaamini tunaendelea kufanyakazi kubwa ya
kupunguza na ikibidi kuondoa kabisa,” alisema Bwanakunu kisha kumkabidhi cheti
cha shukrani mkuu huyo wa mkoa.
0 comments:
Post a Comment