Wakazi wa Mwakata wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga bado wanakubwa na kadhia ya kukosa makazi baada
ya kukubwa na mvua ya mawe iliyoua watu 42 na na kujeruhi 91 mwaka jana
2015 mwezi marchi.
Hayo yamebainishwa Bungeni
na Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige (CCM) alipokuwa akichangia hotuba ya
Rais Dkt. John Magufuli katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika
Baada ya maafa yale kutokea Rais aliyepita Jakaya Kikwete aliagiza
wananchi wale wajengewe nyumba za kuishi ndani ya muda mfupi lakini hadi
tunavyozungumza wananchi wale wanaishi kwenye maturubali jambo ambapo
sii sahihi.
''Ahadi ya Serikali ni
ahadi ambayo inahitaji utekelezaji hivyo namuomba ndugu yangu Jenista
Mhagama Bunge likimalizika twende pamoja jimboni ukajionee hali halisi
ili serikali muanze kuwajengea nyumba wananchi hawa maana wanateseka na
mvua zinazoendelea kunyesha.
0 comments:
Post a Comment