Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga inatarajia kutumia Sh bilioni
15.4 kujenga barabara kwa kiwango cha lami katikati ya mjini huo.
Barabara hizo za katikati ya mji wa Shinyanga, zina kilometa 13.
Tayari ujenzi wa kuziparua, umeshaanza tangu Agosti 24, mwaka jana na
kutarajiwa kukamilika Juni 2018.
Hayo yalizungumzwa jana na Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga, Simon Ngagani kwenye ziara fupi ya Katibu Tawala wa Mkoa huo,
Abdul Dachi wakati akikagua ujenzi wa barabara hizo. Fedha hizo ni
mkopo kutoka Benki ya Dunia. Ngagani alisema ujenzi wa barabara hizo,
utakamilishwa kwa awamu.
Hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wanatarajia kilometa 4.4 zitakuwa
zimekamilika ili kuondoa kero ya upungufu wa barabara katikati ya mji.
Dachi alimtaka mkandarasi anayejenga barabara hizo, Kampuni ya Howard
Humphreys (Ltd), azijenge kwa kiwango kinachotakiwa ili kulingana na
thamani ya fedha na siyo kulipua kazi.
Dachi aliwataka wananchi waliovamia maeneo ya barabara hizo
zinazojengwa, hususan wauza mitumba katika Mtaa wa Sukari, walioamuliwa
waondoke, lakini bado wamekaidi agizo hilo, waondoke kwa hiari yao
wenyewe, kabla Serikali haijatumia nguvu na kuharibu mali zao.
CHANZO ; MTANZANIA.
0 comments:
Post a Comment