Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKAZI wa kijiji cha Mwamandi katika Kata ya Mwanase wilayani hapa,
Marashi Rutaja, aliyefariki dunia juzi, amezikwa na mali zake alizokuwa
akimiliki. Rutaja alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.Enzi za uhai wake, pamoja na mali nyingine, alikuwa akimiliki baa. Akizungumza na gazeti hili, Diwani wa Mwanase, Paulo Samson, alisema enzi za uhai wake, walimhusisha Rutaja na ushirikina na pia kifo hicho kimehusishwa na imani hizo jambo lililofanya wananchi kuamua azikwe na vitu vyake alivyokuwa navyo katika kaburi moja.
Samson alizitaja mali alizokuwa nazo marehemu kuwa ni pamoja na vitanda, magodoro, masanduku ya soda na bia. Alidai aliwasikia wananchi na familia ya marehemu wakisema mali hizo zikibali, zinaweza kuathiri jamii na kijiji hivyo bora zizikwe pamoja na mmiliki.
Samson alisema familia ilieleza kuwa, Rutaja enzi za uhai wake alikuwa akituhumiwa kwa vitendo vya unyang’anyi katika maeneo ya kata hiyo ya Mwanase na kubaki na mali zake ni laana kwao.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment