Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katika mchezo huo, dakika za mwanzo zilionekana kama zingeihakikishia ushindi Simba mapema, kwani Mwinyi Kazimoto na Ajibu walionekana kuisumbua mno ngome ya Kagera. Hata hivyo, umakini wa mabeki wa Kagera uliwezesha kuzua mashambulizi mengi langoni mwao, huku ikifanya mashambulizi machache.
Katika dakika ya 45, Ajib alitumia vizuri pasi aliyopewa na kuweza kuiandikia Simba bao hilo pekee kwenye mchezo huo, ambalo lilidumu hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa na mwamuzi, Mathew Akrama.
Hata hivyo, Kagera katika dakika za majeruhi ilimpoteza mchezaji wake, Daud Jumanne aliyeoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kucheza rafu mbaya. Matokeo hayo sasa yameifanya Simba kufikisha pointi 42 sawa na Azam FC ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Katika mchezo mwingine, Azam nayo iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui lililofungwa na Kipre Tchetche dakika ya 18 na kufikisha pointi 42.
CHANZO: GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment