Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKURUGENZI Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna
amezifunga baadhi ya kumbi za starehe na baa ya Dragoni iliyokuwa karibu
na Shule ya Msingi Town kwa madai kuwa zimekosa viwango vinavyotakiwa
ikiwemo kukosa huduma za vyoo.
Licha ya changamoto hiyo, katika shule hiyo ya msingi ndani ya
madarasa kumekuwa mara kwa mara kukutwa na kondomu ambazo zimekwisha
tumika hali ambayo ni hatari kwa wanafunzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, mkurugenzi huyo
alisema klabu za usiku za Bakurutu maarufu Maduka Mengi, Lubaga Inn na
Butiama zimefungwa mpaka zitakapojirekebisha kwa kutengeneza huduma
zinazotakiwa.
Kalinjuna alisema baa ya Dragon imefungwa moja kwa moja kutoa huduma
kwa sababu ya kutokukidhi viwango hasa kukosa huduma za vyoo na kuwa
karibu ya eneo la shule.
“Hizi baa za usiku zinazokesha zimekuwa na changamoto nyingi hivi
sasa ni suala la usafi kila maeneo wao wanaendesha biashara hizo
pasipokuwa na huduma za vyoo.
Tumeamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha
wasitoe huduma mpaka pale watakapojirekebisha ila baa ya Dragon yenyewe
tumeifungia moja kwa moja,” alisema.
Mkurugenzi wa baa ya Dragon, Humprey Godfrey alisema kitendo cha
kufungiwa kimemsikitisha kwani wakati akianza kufanya biashara hiyo
alipewa leseni kutoka manispaa na kukagua mandhari yake sasa imekuwaje
leo kufungiwa moja kwa moja hilo suala hawajatenda haki.
“Mimi nimeshangazwa na manispaa hii ina maana hawakuona kipindi
wanaponipatia leseni kuwa nipo karibu na shule. Sasa nimeanza biashara
wamekuja kunifungia kwa kueleza makosa mengi hivyo hawajanitendea haki,”
alilalama mkurugenzi huyo.CHANZO: GAZETI LA HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment