Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, 
Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo 
pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka 
litakalofanyika  Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu 
ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na
 baadala yake kufanyika mikoani. 
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.
Msama amesema kuwa 
Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza 
katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.
 Aidha Msama 
amelishukuru  Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika 
Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa 
wingi katika tamasha hilo mkoani humo.
 


 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment