Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amewaonya wanaume
hususani wa maeneo ya vijijini ambao hupenda kuongeza wake kipindi cha
mavuno sababu ya kuchezea chakula na kusababisha baa la njaa kuingia
kwenye familia zao, kitendo ambacho amepiga marufuku.
Matiro alitoa onyo hilo kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ya baadhi
ya wanaume ambao hupenda kuongeza wake wengi pale wanapopata mavuno
mengi, na kusahau kuhifadhi chakula cha kujikimu na pale msimu wa kilimo
unaporejea, huanza kuomba msaada serikalini.
Akizungumza juzi kwenye mikutano mitatu ya hadhara kwa nyakati
tofauti na wanakijiji cha Itwangi, Didia na Imesela katika Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga, Matiro alisema kutokana na mwaka huu kuwa na
neema ya chakula, mwananchi au kijiji kitakachochezea chakula serikali
haitapeleka msaada kwao.
Kwa upande wake, Ofisa Kilimo wa Kijiji cha Ilola, Tarafa ya Itwangi,
Hazina Thomasi aliishauri serikali itunge sheria ndogo ambayo itawabana
wanaume wanaopenda kuuza chakula chote nyumbani kwake, na kuzitumia
fedha kwa matumizi yasiyo rasmi ikiwamo kuoa ovyo na kunywea pombe.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba
alisisitiza wananchi hao kuacha tabia ya kuendekeza kulima mazao ya muda
mrefu ambayo ni bahati kuhimili ardhi ya Shinyanga, bali wawe wanalima
vyakula vya muda mfupi ambao ni mtama, choroko, viazi vitamu angalau
hata ekari moja moja.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Imesela, Hadija Kashindye na James
Kulwa walikiri kuwapo tabia hiyo katika baadhi ya familia wanapopata
mavuno mengi wanaume husahau shida ya chakula na kuuza kwa kuongeza
familia nyingine.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment