Home » » HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA IMETOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI KUMI NA TANO KWA KOSA LA KUTELEKEZA DAMPO LA MJI HUO

HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA IMETOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI KUMI NA TANO KWA KOSA LA KUTELEKEZA DAMPO LA MJI HUO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiizi wa Mazingira Nchini, NEMC limeipiga faini ya shilingi milioni kum na tano Halmashauri ya wilaya ya Kahama kwa kile kinachodaiwa ni uzembe wa kuto zingatia sheria ya mazingira kwa kuliweka Dampo la mji huo katika hali hatashi kwa mazingira na viumbe hai wengine.
Katika Ziara ya Naibu Waziri Mpina Leo Mjini Kahama, ilohusisha ukaguzi wa Dampo, machinjio viwanda na soko la mjini kahama kumebainika kuwa na uzembe kwa watendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wa kutosimamia utupwaji wa taka katika Dampo la mji huo ulohusisha kutupwa kiholela kwa taka ardhini na kuteketezwa kwa njia isiyo salama.
Kufuatia ukiukwaji wa sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake, Baraza la mazingira nchini  NEMC limeshawishika kuitoza faini Halmashauri hiyo ya shilingi milioni kumi na tano na kutakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili.
Akiitaja adhabu hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mkaguzi wa NEMC kanda ya ziwa na Mikoa jirani Bw. Jamali Baruti sambamba na hilo ameleza kuwa, Halmashauri ya Kahama inatakiwa kuboresha miondombi ya taka,kuratibu na kusimamia ujenzi wa mabwawa katika machinjio mjini hapo kwani utupwaji holela wa samadi huchangia uharibifu wa mazingira.
Akitilia msisitizo wa suala zima la uzingatiaji wa sheria ya mazingira kwa watendaji nchini, Naibu Waziri Mpina alisema kuwa hawezi kukubali kuwajibishwa sababu ya viongozi kushindwa kusimamia suala zima la mazingira, na kuhaidi kuwawajibisha viongozi wazembe.
Awali, akitoa taarifa ta usafi wa mazingira ya wilaya ya Kahama Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Nkulu alisema kuwa Kahama imekuwa ikikabiliwa na chngamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni Pamoja na uhaba wa magari ya kuzolea taka, ukataji miti kwa matumizi ya kukaushia tumbaku, na usafishaji wa dhahabu kwa kutumia madini ya zebaki ambayo si rafiki kwa mazingira.
Ziara ya Naibu Waziri  Mpina wilayani Kahama ni Muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
 

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa