Home » » MPINA AINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI YA MJI KAHAMA

MPINA AINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI YA MJI KAHAMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


.
-Maafisa watatu watumbuliwa.

Evelyn Mkokoi na Anceth Nyahore Kahama

SIKU moja baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano
Mazingira Luhaga Mpina,kubaini ukiukwaji mkubwa wa usimamizi wa sheria
za Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)kuiadhibu kulipa
faini ya shilingi milioni 15,jana Naibu Waziri huyo amebaini umwagaji
wa maji taka ovyo katika dampo la tala la Busoka mjini hapa.

Naibu waziri huyo katika ziara yake ya siku ya pili yenye staili ya
kushitukiza na kuachana na ratiba aliyopangiwa, alishuhudia uchafuzi
wa mazigira wa gari moja aina la Fuso lenye namba za usajili T 245 BHC
linalomilikiwa na Shule ya Msingi ya Kwema ya mjini Kahama lililokuwa
likiendeshwa na Johanas Mwambeya,likimwaga maji taka kando ya barabra
karibu na dampo hilo.

Naibu Waziri huyo, aliyekuwa amefauatana na Wakaguzi wa Mratibu wa
NEMC kanda ya Ziwa,Jamal Baruti, alisema kitendo hicho ni hujuma
katika mazingira na ukiukwaji wa kifungu namba 187 cha utunzaji wa
mazingira na kuagiza halmashauri hiyo ndani ya siku saba iwe imechimba
bwawa maalum kwa ajili ya kumwaga maji taka na kutoa adhabu ya mmliki
wa gari hilo kulipa shilingi milioni 1.2 ambazo mmiliki huyo alilipa
mara moja..

“Ni jana tu adhabu ya shilingi milioni 15 imetolewa kwa halmashauri ya mji wa
Kahama kwa ukiukwaji wa usimamizi wa sheria za utunzaji mazingira, na
leo tunashuhudia uchafuzi mkubwa…..tumepita maeneo mengi hatujaona
hali hii ya umwagaji vinyesi tena kando ya barabara na ni mchana
kweupe….umwagaji katika eneo hilo la tambalare kuelekea katika vyanzo
vya maji inasikitisha kweli kweli”Alisema Mpina.

“Hali hii inatafasiriwa kuwa halmashauri au serikali hii ndiyo
inayowapelekea wananchi wake magonjwa ya kuambukizwa kama kipindupindu
na
Typhoid…..huduma nzuri zinazo tolewa na serikali kwa wananchi wake
sasa kwa mlango wa nyuma zinarudia wananchi kwa kuwaumiza….hili
haliwezekani,hakika Mkurugenzi Kahama hili limeonyesha uzembe mkubwa
katika kusimamia usafi wa mazingira na huu sio watumishi wadogo ni
wewe”Alisema Naibu Waziri huyo.

Naibu waziri huyo alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha
uchafuzi mkubwa wa mazingira na hasa mkutitirisha maji machafu yenye
kinyesi katika vyanzo vya maji vilivyo karibu na maeneo ya dampo hilo.

Alisema na kuagiza kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara yake ya siku
mbili wilayani Kahama angependa kusikia na kupata taarifa ndani ya
siku saba kuwa tayari bwawa maalum linachimbwa kwa ajili ya kumwaga
maji machafu.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo, ameiagiza halmashauri hiyo
kuacha mara moja kutupa taka katika uwanja wa wazi maarufu kama uwanja
wa Magufuri uliopo eneo la Majengo mjini Kahama, na kuwa taka zote
zilizopo ziondolewe na eneo la uwanja huo kuwa safi.

Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama
Anderson Msumba,aliahidi kutekeleza agizo la Niabu Waziri huyo, huku
akichukua hatua za kinidhamu za kuwasimamisha kazi baadhi ya maafisa
katika ofisi yake kwa kile alichodai kuwa wakati hali hiyo ikitokea
yeye alikuwa mapumzikoni katika likizo fupi.

Maafisa waliosimamisha kazi ni Mkuu wa Idara ya Usafishaji na
Mazingira,Martin Masele,Afisa Afya na Mazingira Johaness Mwabesi na
Deogratias Dotto Afisa Afya.
Naibu Waziri mpina Pia alitembelea Mgodi wa kuzalisha Dhahabu wa Bulyankulu uliyopo Kahama na kujionea hali ya mazingira mgoni hapo Pamoja na kukagua mabwawa ya kisasa ya kuhifadhi maji taka yatokanayo na uzalishaji kiwandani hapo Mgodi umekuwa ukilalamikiwa na wakazi vya vijiji jirani kuwa wakati wa kipindi cha mvua mabwawa hayo hujaa maji na kwenda kwenye eneo la makazi ya watu na mazingira.
Naibu Waziri Mpina amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC Kujiridhisha malalamiko hayo ya wananchi na kuagiza uongozi wa mgidi kuchukua hatua stahiki pamoja na kurekebisha mapungufu hayo iwapo yatabainika.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa