Na Evelyn
Mkokoi
Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Ukwemi
uliyopo katika wilaya ya Kahama upo hatarini kutoweka kutokana na shughili za kibinadamu zinazofanywa
ndani ya hifadhi hiyo zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Hayo yameelezwa na Meneja kutoka
wakala wa Taifa wa Misitu Bw. Mohamed Dosa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea
HIfadhi hiyo iliyopo ndani ya Halmashauri ya Kahama inayopakana na
Halmashauri ya Mbongwe Mmkoani geita.
Katika Ziara yake ya Ukaguzi wa
Mazingira katika Hifadhi ya Msitu Huo, Naibu Waziri Mpina alielezwa kuwa
shughuli kubwa zinazotegemewa na wakazi wa vijiji vya jirani na msitu huo ni,
ukataji miti kwa uchomaji wa mikaa na ukataji wa magogo kwa shunghuli mbali
mbali ikiwa ni pamoja na shughuli na ujenzi na utengenezaji wa samani za
majumbani.
Meneja Dosa Amemuelezea Naiubu Waziri
Mpina kuwa (generation) kizazi cha
kwanza cha aina na miti ndani ya hifadhi hiyo kilishakwisha na miti inayoota na
kuonekana sasa ni ya kizazi cha pili.
“changamoto kubwa tunayokumbana nayo
katika kulinda hifadhi hii ni magari ya doria kuzunguka ndani ya msitu kwani ni
mkubwa sana na hakuna skari wa kutosha kufanya doria. “ Alisisitiza Bw. Dosa.
Akiwa katikati ya Msitu huo Naibu
Waziri Mpina alijionea Uharibifu mkubwa
wa uchomaji mkaa na kushuhudia mhalifu Bw John Abdalah Sanga makazi wa kijiji
cha jirani cha mwendakulima aliyekuwa akimaliza kuchoma mkaa katikati ya msitu huo na kueleza kuwa amekuwa akifanya
kazi hiyo kwa takribani miaka mitatu sasa hali iliyompelekea Naibu Waziri Mpina
na timu yake kutekekeza baadhi ya matanuru ya mkaa ndani yam situ huo.
Kwa upande wake Mratibu wa Baraza la
Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa Bw. Jamal Baruti
alieleza kuwa hali ya uharibifu wa misitu nchini bado ni kubwa na suala la mkaa
bado ni changamoto, hivyo wanaanchi washiriki katika kuhifadhi misitu na
kutafuta mbadala wa mkaa na misitu ni muhimu kwa kutunza baiyonuwai., wakati
katibu tawala wa wilaya ya kahama Bw. Thomas Nganya akitoa Rai kwa wananchi waone kuwa suala la
utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na siyo kuiachia seriali peke
yake.
0 comments:
Post a Comment