Jumamosi Novemba 26,2016.Hapa ni katika barabara ya Shinyanga- Tabora,maandamano ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Shinyanga ambao ni Jeshi la polisi,Agape,ICS,PACESH,Rafiki,Red cross,ofisi ya mkurugenzi manispaa ya Shinyanga na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa siku 16 za maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani mkoa wa Shinyanga.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wenye kauli mbiu ya ‘Funguka sema hapana kwa ukatili wa kijinsia,elimu salama kwa wote’ alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Takwimu zinaonesha kuwa tatizo la ndoa za utotoni kwa mkoa wa Shinyanga ni 59% ikifuatiwa na Tabora 58% na Mara 55%.
Pia kwa wastani takribani watoto wawili kati ya watano nchini Tanzania wanaolewa chini ya umri wa miaka 18 na kwa mwaka 2010 pekee 37% ya wanawake wenye umri kati ya 20-24 walikuwa wameolewa au walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti wa UNFPA katika wilaya ya Kahama na Kishapu unaonesha kuwa zaidi ya watoto 500 wa kike katika mkoa wa Shinyanga huacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni kila mwaka.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNFPA (2013) asimilia 45 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika mkoa wa Shinyanga na Mwanza kwa kipindi cha mwaka 2010 pekee na 25% ya wanawake mkoani Shinyanga wamefanyiwa ukatili wa kingono.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo kwenye uzinduzi wa siku 16 za maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Shinyanga leo Novemba 26,2016 ametuletea picha 37..Tazama hapa chini.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Shinyanga wakiandamana kutoka ofisi ya afisa Mtendaji kata ya Ibinzamata kuelekea uwanja wa shule ya msingi Ibinzamata katika manispaa ya Shinyanga wakati wa uzinduzi wa siku 16 za maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani mkoa wa Shinyanga.
Maandamano yanaendelea
Siku 16 za harakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa iliyoanzishwa na taasisi ya kimataifa ya wanawake katika uongozi ‘Women Global Leadership Institute’iliyoanzishwa mwaka 1991 nchini marekani kwa nia ya kuamsha ari ya kuzuia na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake kwa kuzingatia haja ya kuleta usawa wa kijinsia.
Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango
Kampeni hiyo ilianzishwa ikiwa ni matokeo ya mauaji ya wanawake yaliyotokea 1960 Mirabele nchini Dominica wakiwa katika harakati za kupinga utawala wa kidikteta wa rais wan chi hiyo Raphael Truijilo na kuhitimishwa tarehe 10 Desemba ambayo ni siku ya kimataifa ya tamko la haki za binadamu ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu kwani ukatili huu ni uvunjwaji wa haki za binadamu.
Wadau wakionesha mabango
Maafisa kutoka dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba bango
Maandamano yanaendelea
Maandamano yanaendelea...kila bango na ujumbe mzito
Waandamanaji wakielekea uwanja wa shule ya msingi Ibinzamata
Tunaandamana....
Waandamanaji wakiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Ibinzamata mjini Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakipokea maamandamano hayo
Waandamanaji wakionesha mabango kwa mgeni rasmi
Mgeni rasmi Josephine Matiro akishikana mkono na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi baada ya kumkabidhi bango
Watoto wakicheza muziki
Mgeni rasmi Josephine Matiro akikagua mabanda ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia.Hapa ni katika banda la Investing in Children and their Societies(ICS).Kushoto ni afisa kutoka ICS Shadia Nurdin akimwelezea mkuu wa wilaya ya Shinyanga shughuli zinazofanywa na shirika hilo
Mgeni rasmi Josephine Matiro akiwa katika banda la Red Cross
Hapa n katika banda la shirika la Rafiki
Mgeni rasmi akiwa katika banda la Rafiki
Hapa ni katika banda la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH)
Wa pili kutoka kushoto ni afisa kutoka dawati la jinsia na watoto lililopo katika jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Joseph Christopher akimwelezea mgeni rasmi Josephine Matiro
Kulia ni Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga Pili Misungwi akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na maafisa kutoka dawati hilo ambalo limepongezwa kwa jitihada wanazofanya katika kuhakikisha ukatili wa kijinsia unabaki historia mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa eneo la tukio
Vijana wakitoa burudani
Mmoja wa wadau akitoa ushuhuda jinsi alivyofanyiwa ukatili wa kijinsia
Meza kuu wakishikana mkono na mwanamke aliyetoa ushuhuda namna alivyofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na mme wake.Wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa shirika la Agape Aids Control Programme,John Myola
Kundi la maigizo maarufu kwa jina la Chap Chap wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia
Afisa kutoka shirika la ICS Shadia Nurdin akisoma risala ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ambapo alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na sheria kinzani,sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto kuolewa chini ya miaka 18.Changamoto zingine alizitaja kuwa ni mila potofu ikiwa ni pamoja na kuenzi ngoma za wakato wa mavuno mathalani ukango,uswezi,bukwilima,samba na nyinginezo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema jeshi la polisi lina majukumu ya kusimamia sheria na mikataba ya kimataifa ambayo inahusiana na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia na watoto lakini hawawezi kusimamia peke yao bali wanahitaji ushirikiano na taasisi zingine na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa ukatili unamalizika katika jamii
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo
Mgeni rasmi Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia duniani mkoa wa Shinyanga ambapo aliwataka akina mama katika jamii kupaza sauti badala ya kunyamaza kimya na kuogopa kutoa ushahidi mahakamani pindi wanapotendewa ukatili katika familia zao huku akiwaasa kukaa karibu na watoto wao ili watoto hao waweze kuwasimulia kama wanatendewa vitendo vya kikatili.
Matiro aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Shinyanga kufungua makanisa na misikiti maeneo ya vijijini ili watu wawe na hofu ya mungu waache kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwataka wananchi wote kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia na watoto
Wanafunzi wa shule ya msingi Ibinzamata wakicheza muziki
Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga Pili Misungwi alisema suala ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa katika jamii hivyo dawati lake linaendelea na jitihada za kuwatafuta,kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Misungwi alisema siku 16 za harakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa iliyoanzishwa kwa lengo nia ya kuamsha ari ya kuzuia na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake kwa kuzingatia haja ya kuleta usawa wa kijinsia.Alisema katika siku hizo 16 wataendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na hata baada ya siku hizo 16,wataendelea na utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi na kuwashughulikia watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment