TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13
Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha
wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.
Rais
Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha
kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.
Rais
Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika
habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea
katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.
''Serikali
ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya
uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya
uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna magazeti mawili tu kila
ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao wanageuza hii nasema na
nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia wasikie wasiposikia
wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa
uchambuzi mzuri sana''.
Rais
Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona amani ya nchi
inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la maendeleo ya
taifa lolote duniani.
Amesema
bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza kuja kuwekeza nchi, hata
wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Rais
Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha wawekezaji wa Kiwanda
cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za chakula nchini na
kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga kujengwa
mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.
Aidha
ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa
mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha
wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha
watanzania waliowengi
Rais
Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa
vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda
vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika
siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu
Shinyanga
13
Januari 2017.
0 comments:
Post a Comment