Hivi karibuni baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga lilitoa azimio kumtaka mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga afuatilie mkataba wa mkandarasi JASCO Investment kumwagilia maji mara tatu kwa siku kwani fedha kwa ajili ya kumwagili barabara ilishatengwa na amekuwa akilipwa.
Ikumbukwe pi kuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro aliwahi kuagiza Mkandarasi JASCO akamatwe kwa kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.
ANGALIA HAPA VIDEO
ANGALIA MATUKIO HAPA CHINI JINSI WALIVYOFUNGA BARABARA
Barabara ya Magadula/Mohamed Trans inayotenganisha kata ya Ngokolo na Ndembezi mjini Shinyanga ikiwa imefungwa kwa mawe na matofali.Hapa ni karibu na ukuta wa kanisa Katoliki la Ngokolo na shule ya msingi Bugoyi B.-Picha zote na Kadama Malunde na Isack Luhende - Malunde1 blog
Muonekano wa barabara
Hili ni eneo jingine ambapo wananchi walifunga barabara hiyo
Baadhi ya wananchi wakiwa katika barabara hiyo wakiwa na mwenyekiti wa mtaa wa Magadula Diana Ezekiel (aliyesimama karibu na bajaji).
Mwenyekiti wa mtaa wa Magadula Diana Ezekiel akitoa maelezo kwa mwandishi wa habari aliyewahi kufika katika eneo hilo,Kadama Malunde kwanini wameamua kufunga barabara.
Mwandishi wa habari Kadama Malunde akichukua maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa wa Magadula Diana Ezekiel
Askari polisi baada ya kufika katika barabara hiyo.
Askari polisi wakiwaita wananchi waje waondoe mawe na matofali hayo
Wananchi waliokuwa karibu na barabara hiyo wakiondoa mawe na matofali baada ya kuitwa na polisi.
Zoezi la kuondoa mawe likiendelea
Askari polisi wakizozana na mwenyekiti wa mtaa wa Magadula Diana Ezekiel kabla ya kumkamata na kumpandisha kwenye gari la polisi,baada ya kumkamata ndipo walimwamuru pia mwandishi wa habari Kadama Malunde apande kwenye gari la polisi.
Kadama Malunde akiwa na kitambulisho chake cha kazi baada ya kutoka kituo cha polisi.
Picha zote na Kadama Malunde na Isack Luhende - Malunde1 blog
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde
anayeandikia gazeti la Mtanzania na Mmiliki wa Mtandao wa Malunde1 blog
amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakati akipiga picha
baada ya wananchi kuziba barabara ya Magadula mjini Shinyanga.Waandishi wetu wanaripoti.
Tukio
hilo limetokea leo Jumatano Agosti 16,2017 majira ya saa tano asubuhi
katika eneo hilo la barabara hiyo baada ya wananchi kuziba barabara hiyo
kwa mawe na matofali wakidai wamechoshwa na vumbi kali linatokana na
mchanga na simenti/saruji baada ya magari kupita eneo hilo.
Malunde
alifika katika eneo hilo kutekeleza majukumu ya uandishi wa habari
baada ya kupata taarifa kuwa wananchi wameziba barabara hiyo ili kuzuia
magari yasipite katika barabara hiyo.
Baada
ya kuwahoji wananchi hao ghafla askari wa jeshi la polisi walifika
katika eneo hilo na kuwataka wananchi waliokuwepo eneo hilo kuondoa mawe
na matofali huku mwandishi huyo akiendelea kupiga picha.
Wakati
anaendelea kupiga picha askari mmoja alihoji kwanini anapiga picha
ndipo Malunde aliposema ni mwandishi wa habari lakini askari huyo
alimtaka atoe kitambulisho cha kazi na wakati anataka kuonesha
kitambulisho alitokea askari mwingine (Mkuu wa kituo cha polisi wilaya
ya Shinyanga) akihoji kwanini anapiga picha na kumwamuru apande kwenye
gari la polisi.
Hali
hiyo ilileta mvutano baina ya mwandishi huyo wa habari na askari polisi
hao na hata alipoonesha kitambulisho mkuu huyo wa kituo cha polisi
alisisitiza apandishwe tu kwenye gari,naye akatii amri hiyo.
Baada
ya kufikishwa katika kituo cha polisi,Malunde alitakiwa kutoa maelezo
ya tuhuma ya kosa la uchochozi akidaiwa kuwahamasisha wananchi kuziba
barabara.
Baada
ya kuandika maelezo hayo askari polisi kitengo cha upelelezi aliyekuwa
anamchukua maelezo kwa agizo la mkuu wa kituo cha polisi alimruhusu
mwandishi huyo kutoka kituo cha polisi na kwamba kama watamhitaji
wamuita kituoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kutoka kituo cha polisi,Malunde alisema
anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi wakati wananchi wakiwa wameziba
barabara.
“Nimeandika
maelezo baada kuambiwa natuhumiwa na kesi ya uchochezi,kwamba
nimehamasisha wananchi waweke mawe na matofali wakati mimi nimefika eneo
la tukio kutekeleza majukumu yangu ya uandishi wa habari”,alisema Malunde.
“Nimefika
eneo la tukio kuandika habari juu ya tukio lililokuwa
linaendelea,nimekuta wananchi wanaendelea kufunga barabara wakiongozwa
na mwenyekiti wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo Diana Ezekiel nikaanza
kuwahoji wakasema wamefunga barabara kwa sababu ya vumbi katika
barabara hiyo”,alieleza Malunde.
“Wananchi
hao walieleza kuwa makubaliano ya mkataba wakati Kampuni ya ukandarasi
JASCO anayesimamiwa na halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ni kwamba
anatakiwa kuwa anamwaga maji asubuhi,mchana na jioni lakini hali imekuwa
tofauti kabisa kwa muda wa zaidi ya miezi sita sasa”,alieleza.
Malunde
alisema baada ya kumaliza kufanya mahojiano na wananchi alikaa pembeni
ili kujua kitakachoendelea na baada ya takribani dakika 10 askari polisi
walifika eneo hilo na kuwataka wananchi waliokuwa eneo hilo kuondoa
mawe na matofali hayo.
Wakati
polisi wakiwa eneo hilo huku wananchi wakiendelea kuondoa mawe
hayo,ghafla askari polisi mmoja alihoji kwanini anapiga picha,alipojibu
ni mwandishi wa habari aliombwa aoneshe kitambulisho wakati anajiandaa
kuonesha ndipo alitokea askari mwingine (OCD) akimtaka apande kwenye
gari la polisi anafanya uchochezi.
“Pamoja
na kwamba nilieleza kuwa ni mwandishi wa habari na kutaka kuwaonesha
kitambulisho cha kazi askari hao waliendelea kunizonga,huku mkuu wa
kituo cha polisi ambaye sikuwahi kumuona aliyejulikana kwa jina la Cloud
Kanyolota akiamuru nipandishwe kwenye gari la polisi kwamba kwanini
nakuwa mbishi,nikauliza kwanini akasema mimi mchochezi,nikaamua kupanda
na kuelekea kituo cha polisi wilaya”,aliongeza Malunde.
Mwandishi
huyo wa habari baada ya kushikiliwa kituoni hapo kwa takribani masaa
mawili kisha kuandika maelezo yake aliruhusiwa kutoka polisi bila
dhamana na kuelezwa kuwa endapo watamhitaji watamwambia.
Akizungumza
kabla ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma ya uchochezi kwa kuwaongoza
wananchi kuziba barabara,Mwenyekiti wa mtaa wa Magadula Diana Ezekiel
alisema barabara hiyo imekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo hali
iliyowafanya wachukue uamuzi wa kufunga barabara hiyo.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alisema mkandarasi
anayejenga barabara hiyo hamwagi maji tatizo linalotokana na
halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kutomsimamia ipasavyo
“Ujenzi
wa barabara unaotokana na pesa za benki ya dunia ulianza Tarehe 1
Julai,2016,ulitakiwa ukamilike ndani ya miezi 6 lakini mpaka sasa
haujakamilika,mbaya zaidi mkandarasi kamwaga simenti hali ambayo
inasababisha vumbi kali na kuhatarisha afya za watumiaji wa barabara hii
na wananchi wanaoishi jirani na barabara hii”,alieleza Ntobi.
“Tunalaani
kitendo cha jeshi la polisi kumkamata mwandsihi wa habari ambaye
akikuwa anatekeleza majukumu yake,lakini pia tunataka jeshi la polisi
limwachie huru mwenyekiti wa mtaa wa Magadula,Diana Ezekiel bali
wamkamate mkandarasi,lakini pia tunatoa siku tano maji yaanze kumwagwa
la sivyo tutaandamana kata nzima”,aliongeza Ntobi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule alisema wamemuachia huru mwandishi huyo wa habari bila masharti.
0 comments:
Post a Comment