Home » » MWENYEKITI WA MTAA ASHIKILIWA NA POLISI KUHAMASISHA VURUGU MTAANI

MWENYEKITI WA MTAA ASHIKILIWA NA POLISI KUHAMASISHA VURUGU MTAANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399


 Wananchi wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga wameifunga kwa mawe barabara inayoendelea kujengwa na kampuni ya ukandarasi ya Jasco Investment, kwa madai ya kuchoshwa na vumbi.
Pia Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde na mwenyekiti wa mtaa huo Diana Ezekiel wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Wananchi hao walifanya tukio hilo jana saa tano asubuhi katika eneo hilo huku wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa huo, wakidai kuchoshwa na vumbi kali linatokana na mchanga na saruji baada ya magari kupita eneo hilo. 
Wakati Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari akishikiliwa kwa muda wa saa mbili na kuachiwa kwa madai ya kupiga picha tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa anashikiliwa kwa madai ya kuhamasisha wananchi kufunga barabara.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule alisema walikamatwa watu wawili akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo na mwanamume mmoja akipiga picha.
“Huyo mwananume mwingine alipofikishwa kituoni akahojiwa alijitambulisha kama mwandishi wa habari hivyo akaachiwa bila masharti lakini mwenyekiti wa mtaa huyo bado tunamshikilia,” alisema Kamanda

Chanzo Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa