Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza wakati wa kampeni ya afya aliyoizindua kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani ambaye pia mganga mkuu wa wilaya akizunguza wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Maguja Daniel akitoa neno wakati wa uzinduzi huo.
Na Robert Hokororo, Kishapu DC.
Wananchi
wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Afya (CHF) iliyoboreshwa ili wapate
huduma na kuboresha afya zao na hivyo kuweza kushiriki shughuli
mbalimbali za uzalishaji.
Wito
huo ulitolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese
wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji shughuli za afya wilayani
hapa.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo katika kijiji cha Malwilo, Mheshimiwa
Nyabaganga Taraba, Kangese aliwataka viongozi wa serikali za vijiji
kuonesha mfano kwa kujiunga na mfuko huo mapema.Kangese
pia aliwataka viongozi hao kuhamasisha kaya zingine zijiunge ifikapo
Oktoba mwaka huu wakiwemo walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF).
Alisema
huduma hiyo ni muhimu kwa wananchi wasiojiweza na wenye kipato cha
chini ambapo kwa sh. 10,000 humuwezesha kuhudumiwa yeye na watu wengine
sita katika kaya kwa mwaka mzima.
Alisema
Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kutengeneza
miundombinu, kutoa vifaa tiba na kuongeza wataalamu wa sekta hiyo ili
waweze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.Katibu
Tawala huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa CHF iliyoboreshwa
ulianza rasmi Machi 2016 kwa kuimarisha mfumo wa fedha na uoreshaji dawa
na vifaa tiba.
0 comments:
Post a Comment