Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shirika
la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga leo
Jumanne Agosti 15,2017 limezindua Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za
watoto na utawala utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili katika
kata 30 kwenye halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini
na Kahama Mji.
Wa
kwanza kushoto ni Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John
Nhabi,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a na Meneja wa
Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima (wa kwanza
kulia) wakiwa katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga wakati wa
uzinduzi wa mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa
na Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la
kuhudumia watoto “Save The Children International” kwa hisani ya shirika
la Maendeleo la nchini Sweeden – SIDA.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Wadau
mbalimbali wa masuala ya watoto kutoka kata 30 za halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga Vijijini,Manispaa ya Shinyanga na Kahama Mji ambako mradi
huo utatakelezwa
wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi
wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala.
Mkurugenzi
wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akieleza namna mradi huo
utakavyosaidia kupunguza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.
Mkurugenzi
wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza ukumbini ambapo
alisema ili kufanikisha mradi huo pia panahitajika bajeti kutoka
serikalini kwa ajili ya watoto.
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Meneja
wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima
akieleza namna wanavyoshirikiana na serikali katika kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo katika jamii.
Wadau wakiwa ukumbini.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akisisitiza jambo.
Afisa
Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John Nhabi akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mradi huo ambapo alisema jitihada za maksudi zinahitajika
ili kukabiliana na tatizo la watoto wa kiume kulawitiwa na watu wazima
lakini pia wao kwa wao.
Maafisa watendaji wa kata wakiwa ukumbini.
Meneja
Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la
Rafiki SDO,Shangwe Kimath akitambulisha mradi huo ukumbini.
Mratibu
wa Masuala ya Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka shirika
la Rafiki SDO,Alex Enock akichangia hoja ukumbini
Diwani
wa kata ya Lubaga,Mchungaji Obeid Jilala (Chadema) akichangia hoja
ukumbini ambapo alihamasisha mashirika yanayotekeleza miradi katika
jamii kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ipasavyo.
Diwani
wa kata ya Ndembezi,David Nkulila (CCM) akichangia hoja kuhusu namna ya
kulinda haki za watoto ambapo alisema Mikopo imekuwa ikiwanyima haki
watoto pale panapotokea wazazi/wakopaji kufirisiwa mali nyumbani huku
akisisitiza suala la umiliki wa mali katika familia linahusu pia
watoto,hivyo wazazi wanapofirisiwa watoto wanapoteza haki zao.
Diwani
wa kata ya Kambarage,Hassan Mwendapole ( CCM) akichangia hoja ukumbini
ambapo aliwataka wazazi na walezi kuwajali watoto wao kwa kuwapatia
mahitaji muhimu ili kuwaepusha kutojiingiza katika vitendo viovu.
Mwendapole aliwataka wazazi kuwanunulia watoto wao nguo za ndani 'Chupi'
kwani kutokana na kujisahau kwao kunasababisha watu wenye tabia mbaya
kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto matokeo yake wanajiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi wangali wadogo hatimaye wanapata ujauzito na hata
kuambukizwa magonjwa ya yanayotokana na ngono.
Diwani
wa kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi akichangia hoja ukumbini ambapo
alisisitiza serikali kutenga bajeti kwa ajili ya watoto,huku akibainisha
kuwa halmashauri ya wilaya imekuwa ikidai kutenga bajeti lakini
haiwafikii walengwa.
Mwanafunzi
Zuhura Juma kutoka shule ya msingi Ushirika katika manispaa ya
Shinyanga akizungumzia umuhimu wa watoto kupewa haki zao.
Mwanafunzi
Jenifa Maganga kutoka shule ya Msingi Bugoyi A katika manispaa ya
Shinyanga akichangia hoja ukumbini ambapo alisisitiza umuhimu wa wazazi
kujali watoto wao na kuwasikiliza.
Mwanafunzi,Faraja Kichele kutoka shule ya Msingi Ushirika katika manispaa ya Shinyanga akichangia hoja ukumbini.
Mwalimu Faustina Mram kutoka shule ya msingi Bugoyi A akichangia hoja ukumbini kuhusu namna ya kuwalinda watoto.
Afisa Maendeleo manispaa ya Shinyanga,Mwanamsiu Dossy akichangia hoja ukumbini.
Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Shinyanga,Beatrice Mbonea akichangia hoja ukumbini.
Diwani
wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza wakati uzinduzi wa mradi
wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala. Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
Uzinduzi
wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga
ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro.
Akizungumza
wakati wa kuzindua mradi huo,Matiro alilitaka shirika hil0 kushirikiana
na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa jadi la
sungusungu,serikali,viongozi wa dini,kimila na wananchi. “Niwapongeze
sana Rafiki SDO kwa kupata mradi huu muhimu kwa ajili ya ulinzi wa
watoto,sote tunatambua kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vimekithiri
katika jamii,serikali pekee haiwezi kumaliza vitendo hivi,lazima
tushirikiane ili watoto wetu wawe salama”,alisema Matiro.
“Natamani
kusikia mashirika yanajitokeza kuanzisha miradi kwa ajili ya kupambana
na vitendo vya ulawiti wanavyofanyiwa watoto wetu,taarifa nilizo nazo ni
kwamba baadhi ya watoto wa kiume waliopo katika shule za msingi
wanafanyiwa mchezo mbaya wa kulawitiwa,tena wanafanyiwa na watu
wazima,hili halikubaliki lazima tushirikiane kumaliza tatizo
hili”,aliongeza Matiro.
“Naomba
mashirika yanayojihusisha na masuala ya watoto yajitokeze na kuanzisha
miradi ya kusaidia watoto wanaolawitiwa,tunapaswa kuwalinda watoto
hawa,kinachotakiwa ni ushirikiano japo changamoto katika kesi za ukatili
ni wazazi na walezi kumaliza kesi kienyeji”,alisema Matiro.
Katika
hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano katika
vyombo vya dola pale panapotokea watoto wamefanyiwa vitendo vya kikatili
na kunyimwa haki zao.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard
Ng’ong’a alisema mradi huo unatekelezwa na Shirika la Rafiki SDO kwa
kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto “Save The
Children International” kwa hisani ya shirika la Maendeleo la nchini
Sweeden – SIDA.
Ng’ong’a
Mradi huo unalenga kumlinda mtoto na kuhakikisha watoto wanapata haki
zao pamoja na kuwajengea uwezo wa kupaza sauti zao ili kuhoji haki hizo
kutoka kwa wazazi, viongozi na wadau wengine wanaohusika.
“Kupitia
mradi huu,tunaamini vitendo vya ukiukwaji wa haki za watoto
vilivyokithiri mkoani Shinyanga vitapungua kwa asilimia 20% katika kata
30 za Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga vijijini na Mji wa Kahama ifikapo
mwezi wa Novemba mwaka 2018”,alisema Ng’ong’a.
Aidha
alisema mradi huo utasaidia kuongeza utumiaji wa mifumo rasmi kama vile
ofisi za ustawi wa jamii, dawati la jinsia na watoto pamoja na vituo vya
huduma viliyowekwa na serikali na wadau wengine katika kumlinda mtoto
na haki zake.
“Tunatarajia
pia ongezeko la ushiriki wa watoto katika kutoa maamuzi, kuhoji na
kudai haki zao kutoka kwa wazazi na wadau wengine wanaopaswa kuwahudumia
watoto”,aliongeza Ng’ong’a.
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala
kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema ili kufanikisha
mradi huo ipasavyo wamejipanga kutoa mafunzo na kuongeza uelewa wa
ulinzi wa mtoto kwa jamii, kuhamasisha ushirikishwaji wa mtoto na
uragbishi na ushawishi.
“Pamoja
na mambo mengine tumeandaa kampeni za kuhusisha wanaume katika malezi
na makuzi ya watoto na kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa
serekali za mitaa, wazazi, waalimu na kamati za ulinzi wa mtoto juu ya
ulinzi wa mtoto na utawala wa haki za watoto”,alieleza Kimath.
Naye
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima
alisema mradi huo unatekelezwa katika mikoa mitatu nchini
Tanzania,ambayo ni Shinyanga,Dar es salaam na Songwe. “Tunaishukuru
serikali kwa kuendelea kushirikiana nasi katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali,tunampongeza mkuu wa wilaya Josephine Matiro kwa ushirikiano
wa kutosha ambao amekuwa akitupatia,suala la ulinzi wa motto linahitaji
ushirikiano wa wadau wote”,aliongeza Malima.
Mradi
huo utatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwenye kata
ya Ngokolo, Ndembezi , Masekelo Ndala, Kambarage, Ibinzamata Chamaguha,
Chibe, Lubaga na Old Shinyanga na katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga ni kwenye kata ya Salawe, Lyamidati, Mwenge, Mwantini, Tinde,
Didia, Solwa, Iselamagazi Lyabusalu na Lyabukande.
Kwa
upande wa halmashauri ya Mji wa Kahama mradi utatekelezwa kwenye kata ya
Mwendakulima, Nyihogo, Kagongwa, Nyasubi, Majengo, Kahama mjini,
Mhongolo Zungomela, Nyandekwa na Busoka.
0 comments:
Post a Comment