Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkoa
wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya
siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe
11 mwezi Oktoba.
Maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika mkoa wa Shinyanga
yamefanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga Vijijini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab
Telack.
Sherehe
za maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike yamehudhuriwa na watoto
kutoka maeneo na shule mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa serikali
na vyama vya siasa,wananchi na mashirika na taasisi zisizokuwa za
kiserikali likiwemo shirika la kimataifa la Save the Children.
Maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mwaka huu yamebebwa na kauli
mbiu ya “Tokomeza Mimba za utotoni,Tufikie uchumi wa viwanda”.
Akitoa
hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,Josephine Matiro alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa
mikoa mitano inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini hivyo jitihada
mbalimbali zinahitajika kuhakikisha mimba za utotoni zinatokomezwa
mkoani humo.
“Ili
tufikie uchumi wa viwanda tunahitaji kutokomeza mimba za utotoni ambazo
zinachangiwa pia na ndoa za utotoni,ni wajibu wetu serikali,wazazi na
wadau wote yakiwemo mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya haki
za watoto kuweka nguvu pamoja ili kukomesha vitendo hivi”,alieleza
Matiro.
Aidha
aliwanyoshea vidole baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakishirikiana na
wanaume wanaowapa mimba watoto kwa kumaliza kesi kimya kimya huku
wengine wakidiriki kuozesha watoto.
Matiro
alitumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la jadi sungusungu kuwashughulikia
watu wanaowapa mimba watoto huku akitaka elimu zaidi kuendelea kutolewa
katika jamii kuhusu haki za watoto.
Matiro
pia aliwasisitiza wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kike na
kuwaeleza madhara ya kujiingiza katika mambo ya mapenzi wangali wadogo
badala ya kuwaonea aibu huku akiwataka watoto kutokubali kudanganywa na
waume ili kuepuka mimba za utotoni.
Naye
Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa
Shinyanga,Benety Malima alisema vitendo vya mimba na ndoa za utotoni
litapungua endapo kesi zinazohusu masuala ya watoto zitachukua muda
mfupi kumalizika.
“Bado
tuna tatizo la mifumo ya utoaji haki,matukio ya ukiukaji wa haki za
watoto yanapotokea,mara nyingi vyombo vya dola ikiwemo polisi wamekuwa
wakitumia muda mrefu kufanya uchunguzi,hali hii inatoa mwanya kwa
wahalifu kuwapa hongo wazazi watoto kisha kumaliza kesi kienyeji na haki
ya mtoto kupotea”,alieleza Malima.
Hata
hivyo Malima alishauri kuanzishwa mfumo maalumu kutoa elimu kwa jamii
kuhusu haki za watoto utakaosimamiwa na serikali kwa kuyahusisha
mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto ili jamii iweze
kuondokana na mila potofu zinazogandamiza haki za watoto.
Kwa
upande wake,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal
aliwataka akina mama kuwa mstari katika kuhakikisha watoto wanaenda
shule na kukataa watoto wao kuozeshwa kwa tamaa ya mali huku
akiwasisitiza watoto kusoma kwa bidii na kutokubali kurubuniwa kuacha
masomo ama kuambiwa wafanye vibaya katika mitihani yao ili wakifeli
waolewe.
Akisoma
risala kwa niaba ya watoto wa kike mkoa wa Shinyanga,Rosemary Richard
kutoka shule ya msingi Iselamagazi alisema miongoni mwa changamoto
zinazowakabili watoto ni jamii kuwa na uelewa mdogo kuhusu haki za
watoto.
Alizitaja
changamoto zingine kuwa ni mila potofu,watoto kutoshirikishwa katika
maamuzi na kutoa mawazo katika familia,kubakwa,kupewa mimbana kukatishwa
masomo ili wawe chanzo cha mapato wanapoolewa.
Aliiomba
serikali na wadau kutoa elimu kuhusu haki na sera za mtoto huku
akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali watu wanaowafanyia ukatili
watoto lakini pia akaomba katika kila shule kutenga vyumba maalum kwa
ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi.
Mgeni
rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Zainab Telack,akitoa hotuba katika kata ya Iselamagazi
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini leo Oktoba 11,2017.Picha
zote Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma
kwa bidii na kukataa kurubuniwa ili kuepuka mimba za utotoni.
Watoto wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro huku wakisoma vipeperushi vinavyohusu masuala ya watoto.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.
Mgeni
rasmi Josephine Matiro (katikati ya watoto) akicheza muziki na
wanafunzi,aliyevaa nguo nyekundu ni Afisa Utamaduni wa wilaya ya
Shinyanga,Janeth Elias,aliyekuwa MC katika maadhimisho hayo ya siku ya
mtoto wa kike.
Meneja
wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety
Malima akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa
kike kwa mkoa wa Shinyanga ambapo alisema mapambano dhidi ya mimba na
ndoa za utotoni yanahitaji ushirikiano baina ya serikali,wazazi na
mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto.
Wanafunzi wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.
Meneja
wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety
Malima aliwataka wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na
wakati ikiwemo ya Chagulaga ambayo wanaume hutumia fursa kuchagua
mchumba na kusababisha watoto wa kike waolewa bila ridhaa yao.
Meneja
Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la
Rafiki SDO,Shangwe Kimath akitoa neno wakati wa maadhimisho ya siku ya
mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Ngassa Mboje akizungumza
katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari Iselamagazi wakiimba na kucheza wakati wa
maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
Mtoto akiwa ameshikilia bango lililobeba ujumbe.
Awali Watoto wakiandamana na mabango wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike.
Watoto wakiwa wameshikilia bango.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal (CCM) akizungumza katika
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambapo aliwasihi
wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwa ndiyo urithi pekee unaofaa
kwa watoto na kuwataka waache kuozesha watoto kwani wanawanyima haki
zao.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal aliwaomba wazazi kuwa
karibu na watoto wao ili waweze kuwaeleza matatizo wanayokutana nayo
Wadau wakiwa eneo la tukio.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal akicheza na watoto.
Wananchi wa Iselamagazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakicheza muziki.
Wadau kutoka taasisi na mashirika mbalimbali yanayohusika na masuala ya watoto wakiwa eneo la tukio.
Watoto wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa maadhimisho hayo.
Burudani ya Ngoma ya Mabulo ya Jeshi kutoka kundi linaloongozwa na Msanii wa Nyimbo za asili Wanzigiza ikiendelea.
Afisa
Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akielezea kuhusu hali
ya mimba za utotoni mkoani Shinyanga,ambapo alisema mkoa wa Shinyanga
unashika nafasi ya tano kwa mimba za utotoni kwa asilimia 34 ambapo mkoa
wa kwanza ni Katavi (45% ,Dodoma (43%),Tabora (39%) na Mara (37%).
Wanafunzi wakiimba kwaya
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa yakiendelea.
Watoto wa kiume wakiimba wimbo kuwaasa watoto wa kike kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Mtoto Rosemary Richard akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Watoto
wakiwa wameshikilia katarasi zenye maandishi yanayoonesha
matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike kabla ya Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzichoma kama ishara ya
kupinga vitendo hivyo.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Afisa Maendeleo ya Jamii
mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakichoma moto katarasi zenye maandishi
yanayoonesha matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike.
Karatasi hizo zikiwaka moto.
Wadau wakiwa katika eneo la tukio.
Watoto wakicheza mchezo wa igizo kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Meza kuu wakifuatilia kwa umakini igizo la watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni.
Wimbo kutoka kwa wananchi wa Iselamagazi ikiendelea.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu
katika shule ya Msingi Iselamagazi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Zainab Telack.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti.
Picha ya pamoja ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na wadau baada ya kupanda mti.
Walimu
wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya
mti uliopandwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba
ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Wanafunzi wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Shirika la Save the Children
Wanafunzi wakifurahia.
Picha ya kumbukumbu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment