Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akizungumza na wananchi
wakati wa zoezi la kukabidhi hati za kimila katika kijiji cha Negezi
kata ya Ukenyenge.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akikabidhi moja ya hati za kimila kwa mwananchi katika kijiji cha Negezi.
Meneja
wa na Shirika la Misaada ya Kijamii (REDESO), Charles Buregeya
akionesha moja ya hati miliki za kimila kwa wananchi waliofika kwa ajili
ya kukabidhiwa kijiji cha Negezi.
Afisa
Mipango Miji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Celestine
Mwizarubi akitoa malekezo kuhusu hatua za utoaji wa hati za kimila
wakati wa hafla ya makabidhiano.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu akitoa neno wakati wa hafla hiyo.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akikabidhi hati ya kimila kwa mwananchi katika kijiji cha Negezi.
Mgeni
Rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese (wa pili kulia
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa hati za kimila
na maafisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu.
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu ikishirikiana na Shirika la Misaada ya Kijamii
(REDESO) imekabidhi hati 43 za kimila za ardhi kwa wananchi katika
kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge.
Hati
hizo zimekabidhiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese
kwa wananchi hao ikiwa ni sehemu ya jumla ya hati 87 ambazo
zinatarajiwa kutolewa katika kijiji hicho.
Kengese
aliwataka wananchi hao kuzitumia hati kwa kuboresha hali zao kiuchumi
kwa kukopa katika taasisi za kifedha na kuanzisha miradi mbalimbali ya
maendeleo na kujipatia kipato.
Alisisitiza
kilimo chenye tija katika ardhi hizo ambapo aliwataka kufuata kanuni
bora za kilimo ili kupata mavuno kwa kiasi kikubwa ambapo wataipa
thamani ardhi wanayomiliki.
Aidha,
alisema pamoja na hayo pia wananchi wanapaswa kupanda miti ili kutunza
mazingira kwani ardhi iliyotunzwa kwa kupandwa miti ina thamani kubwa
zaidi ya ile isiyokuwa na mti hata mmoja.
Kwa
upande mwingine Katibu Tawala huyo aliwataka wananchi waliokabidhiwa
hati hizo kuwahamasisha wanajamii wenzao kuona umuhimu wa kupata hati za
kimila za kumiliki ardhi katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment