Rahel Madundo akifurahia ushindi baada ya kutangazwa kuwa amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
***
Wanaharakati
wa masuala ya kijinsia kutoka katika vituo vya taarifa na maarifa
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao
wamefanya Mkutano Mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na maarifa katika
wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na baraza la kituo cha taarifa na
maarifa la wilaya hiyo.
Mkutano
huo wa siku mbili ulioanza Novemba 4,2017 hadi leo Jumapili Novemba
5,2017 umefanyika katika ukumbi wa Sheli ya BM kata ya Maganzo wilayani
Kishapu.
Mbali
na mkutano huo kuhudhuriwa na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa
kutoka kata saba,pia umehudhuriwa na maafisa watendaji wa kata pamoja na
baadhi ya madiwani kutoka wilayani Kishapu.
Mkutano
huo ulikuwa na lengo la kupanga mikakati na kuendeleza vituo vya
taarifa na maarifa na kuunda baraza la kituo la wilaya ambapo wajumbe
wa mkutano huo walichagua viongozi wa mtandao wa wilaya ambao kazi yao
ni kusimamia shughuli zote za vituo vya taarifa na maarifa kwa wilaya
hiyo ya Kishapu.
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
uliofanyika katika mkutano huo,John Myola alimtangaza bi Rahel Madundo
(aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kipindi kilichopita) kuwa
mwenyekiti wa baraza hilo kwa muda wa miaka miwili.
Pia
alimtangaza Bi Kayaya Rashid kuwa makamu mwenyekiti,Peter Nestory kuwa
katibu mkuu,Renatus Mahona katibu msaidizi,Hellen Samson mhasibu na
Gayunga James,Pendo Michael,Scolastica Joseph na Agnes Lutamula kuwa
wajumbe wa kamati ya utendaji.
Viongozi
wengine ni Catherine Revocatus aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa
vijana wilaya ya Kishapu,Suzana Yohana kuwa Katibu,Paul Masamaki kuwa
mwakilishi wa kanda ya Mondo,Kulwa Jandikile kanda ya Negezi na Edward
Charles kanda ya Kishapu.
Akizungumza
katika mkutano huo,Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka
TGNP Mtandao,Deogratius Temba alisema vituo vya taarifa na maarifa
vimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa matukio ya ukatili wa
kijinsia.
“Tulianza
harakati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani Kishapu
mwaka 2012,katika maeneo ambapo kuna vituo vya taarifa na maarifa,jamii
imejitambua ambapo wananchi wamejitambua na wamekuwa na ujasiri wa
kupinga vitendo hivi lakini pia wanawake wamekuwa na ujasiri wa kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi”,alieleza Temba.
Temba
alibainisha kuwa wanaharakati wa masuala ya kijinsia kwa kushirikiana
na madiwani wamechangia kwa kiasi kikubwa kuihamasisha halmashauri ya
wilaya ya Kishapu kuwa na bajeti yenye jicho la kijinsia.
“TGNP
Mtandao inawapongeza sana viongozi wa vituo pamoja na madiwani kwa
jitihada wanazofanya katika kuifanya halmashauri ya wilaya ya Kishapu
kuwa mfano wa kuigwa katika kusimamia na kutetea masuala ya
kijinsia”,aliongeza Temba.
Naye
Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel
Madundo,alisema tangu kuanzishwa kwa vituo hivyo mwaka 2012 wilayani
humo,wanaharakati wameisadia jamii kujitambua na kuanza kudai haki zote
za binadamu pamoja na kuingia katika vikao vya kata (WDC).
“Akina
mama wamejengewa uwezo wa kuongea kwenye mikutano ya hadhara na
kuhudhuria mikutano mbalimbali kuomba nafasi za uongozi”,alisema
Madundo.
Aidha
alilishukuru shirika la TGNP Mtandao kwa kuwapatia elimu ya uraghabishi
ambayo imewasaidia kujitambua huku akiliomba shirika hilo kuongeza
vituo vingine katika wilaya hiyo kwani sasa vipo saba pekee.
Katika
hatua nyingine aliiomba halmashauri ya wilaya ya Kishapu kuvipatia
mikopo vituo vya taarifa na maarifa kwa ajili ya kujiendesha na
kuanzisha miradi.
Nao
wajumbe wa mkutano huo walikubaliana kuwa kila shule ya msingi wilayani
humo iwe na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri
wanapokuwa katika hedhi ambapo waliahidi kushiriki katika ujenzi wa
vyumba hivyo.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa shirika linajihusisha na masuala ya haki za
watoto na wanawake la Agape Aids Control Programme,John Myola
aliyealikwa kushiriki mkutano huo,aliwataka viongozi wa vituo vya
taarifa na maarifa na madiwani kuendeleza ushirikiano walionao katika
kuwatetea watoto na wanawake na kuepuka kutumiwa na wanasiasa wenye nia
mbaya.
“Bado
matukio ya ukatili wa kijinsia yapo,watoto wanabakwa,wanapewa
mimba,tafadhali fanyeni kazi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi katika
kutetea wanyonge,kuweni na ushirikiano,tunzeni siri ili kutowapa mwanya
wahalifu,lakini pia jitahidini kutoa taarifa mahali panapohusika kwa
wakati”,alieleza Myola.
Naye
Diwani wa kata ya Mwaweja,Makanasa Kishiwa alilishukuru shirika la TGNP
mtandao kwa kuichagua halmashauri ya Kishapu kuwa miongoni mwa
halmashauri 28 ambako vituo vya taarifa na maarifa vimeanzishwa na
kuahidi kuwa madiwani wataendelea kuungana na shirika hilo katika
jitihada za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Harakati
za TGNP Mtandao wilayani Kishapu zilianza mwaka 2012 katika kata ya
Songwa na baadae kuzaa vituo vya Kishapu,Mondo,Ukenyenge,Mwaweja,Mwadui
Lohumbo na kata ya Maganzo na mpaka sasa kuna jumla ya vituo 7 katika
wilaya hiyo.
Lengo
kuu la kituo cha taarifa na maarifa ni kutoa elimu kwa jamii
nzima,zikiwemo elimu ya kudai rasilimali za umma,ukatili wa
kijinsia,mimba za utotoni na haki za binadamu.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Afisa
Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius
Temba akizungumza katika Mkutano mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na
maarifa katika wilaya ya Kishapu leo Jumapili Novemba 5,2017 katika
ukumbi wa sheli ya BM uliopo katika kata ya Maganzo wilayani
Kishapu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa
Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius
Temba akiwasisitiza wanaharakati wa masauala ya kijinsia kuongeza nguvu
kukabilina na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini
Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius Temba
Mwenyekiti
wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo
akizungumza katika mkutano mkuu mwaka 2017 wa vituo vya taarifa na
maarifa katika wilaya ya Kishapu.
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Rahel Madundo
Aliyekuwa katibu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu Samwel Kalima akizungu
Diwani
wa kata ya Mwaweja,Makanasa Kishiwa akizungumza katika mkutano ambapo
alilishukuru shirika la TGNP mtandao kwa jitihada mbalimbali
linalozifanya katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani
Kishapu
Diwani
wa viti maalumu kata ya Bunambiyu Helena Paul akizungumza ukumbini
ambapo alisema vituo vya taarifa na maarifa vimewasaidia wanawake
kujitambua na sasa kuna viongozi wanawake katika ngazi mbalimbali
wilayani humo wakiwemo madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu
uliopita waliowagaragaza wanaume katika uchaguzi huo mkuu wa mwaka 2015
Afisa
Mtendaji wa kata ya Ukenyenge,Chief Ng'ombe akizungumza kwa niaba ya
maafisa watendaji wilayani humo ambapo aliwataka wanaharakati wa haki za
binadamu kuendelea kushirikiana na serikali katika kupiga vita vitendo
vya ukatili wa kijinsia
Mwenyekiti
wa Mkutano huo,Abdul Mohammed Ngolomole ambaye ni diwani wa kata ya
Songwa akimkaribisha Mkurugenzi wa uchaguzi wa baraza la kituo cha
taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu uliofanyika katika mkutano huo,John
Myola ili kutoa utaratibu wa namna ya kuchagua viongozi wapya wa baraza
la kituo la wilaya ya Kishapu.
Kulia
ni Mwenyekiti wa Mkutano huo,Abdul Mohammed Ngolomole ambaye ni diwani
wa kata ya Songwa akimkabidhi vifaa vya uchaguzi Mkurugenzi wa uchaguzi
wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu,John Myola
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
,John Myola akizungumza wakati wa kutangaza majina ya wagombea wa
nafasi mbalimbali katika baraza hilo
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa baraza la kituo cha taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
,John Myola akielezea utaratibu wa kupiga kura
Wasimamizi wa uchaguzi wakigawa karatasi za kupigia kura baada ya
wagombea wa nafasi mbalimbali ( hawapo pichani) kuomba kupigiwa kura
Wajumbe wa mkutano wakiweka kura zao kwenye ndoo
Rahel Madundo akifurahia ushindi baada ya kutangazwa kuwa amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu kwa kipindi kingine cha miaka miwili
Rahel Madundo akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kumchagua tena kuwa Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
Bi Kayaya Rashid akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa makamu Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu.Kushoto ni Hellen Samson aliyechaguliwa kuwa mhasibu,kulia ni Rahel Madundo aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa wilayani humo.
Peter Nestory akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa katibu mkuu wa vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu.
Picha ya pamoja: Viongozi waliochaguliwa kuongoza baraza la vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
Viongozi wa baraza la vituo vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu
Picha ya pamoja: Viongozi waliochaguliwa kuongoza baraza la vituo vya
taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu,madiwani wa halmashauri ya wilaya
ya Kishapu, Afisa Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP
Mtandao,Deogratius Temba na Mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola
Picha ya pamoja : Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Afisa
Programu – Ujenzi wa nguvu ya pamoja kutoka TGNP Mtandao,Deogratius
Temba na Mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment