Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Novemba 4,2017
amefungua mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa
wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) mwaka 2017.
Mkutano huo mkuu wa SPC ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali
ya kujenga klabu na masuala kadha kadha kuhusu tasnia ya habari.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Katemi Hotel
mjini Shinyanga,Matiro alisema kalamu ya mwandishi wa habari ni fimbo
hivyo kuwataka wazitumie vyema kwa ajili ya maendeleo katika jamii.
Alisema kutokana na kwamba waandishi wa habari ni wadau wakubwa wa
maendeleo ni vyema wakawa wazalendo kwa kutangaza fursa za maendeleo
katika mkoa wa Shinyanga.
“Serikali inatambua mchango wa waandishi wa habari,naomba tushirikiane
katika kuwaletea maendeleo wananchi,sisi viongozi wa serikali
tutaendelea kuwahamasisha wakurugenzi katika halmashauri za wilaya
kuwapa taarifa sahihi pale mnapohitaji”alieleza Matiro.
Katika hatua nyingine aliwaasa waandishi wa habari kujiendeleza kielimu
ili kuongeza umahiri na ufanisi katika kazi zao lakini pia kukabiliana
na sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 inayotaka mwandishi wa
habari awe na kiwango cha elimu kuanzia ngazi ya diploma.
Matiro aliwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari za maendeleo ya
mkoa wa Shinyanga huku akiwaomba kutangaza fursa za uwekezaji katika
viwanda kuunga mkono jitihada za serikali katika kuifanya Tanzania kuwa
ya viwanda.
“Tutakuwa na kiwanda cha nyama katika manispaa ya Shinyanga hivi
karibuni,kutokana na kuwa na kiwanda hicho kinahitajika kiwanda kingine
cha ngozi,naomba wadau kuja kuwekeza katika kiwanda cha
ngozi”,aliongeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga,Kadama Malunde waandishi wa habari mkoani humo wanaunga mkono
jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya
Mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo
wananchi.
“Waandishi wa habari ni daraja kati ya serikali na wananchi,hivyo
kupitia kalamu zetu tupo tayari na tumekuwa tukishirikiana na viongozi
wa serikali kufanikisha utekelezaji wa sera mbalimbali ikiwemo hii ya
kujenga uchumi wa viwanda”,alisema Malunde.
“Ili kufanikisha haya,waandishi wa habari tunaomba ushirikiano kutoka
katika mamlaka mbalimbali zinazohusika kwani baadhi ya viongozi wa
serikali hawapendi kushirikisha vyombo vya habari katika kutekeleza
mambo yanayogusa jamii”,aliongeza.
Aidha Malunde aliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili ya uandishi wa habari na sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya
huduma za habari mwaka 2016 ambayo imekuwa mwiba kwa uhuru wa vyombo vya
habari.
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Mwenyekiti
Kadama Malunde (wa pili kutoka kushoto,akifuatiwa na Katibu Mtendaji
Stephen Wang'anyi na katibu Msaidizi Ali Lityawi) wakimpokea mgeni rasmi
ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro (kushoto) ili
kushiriki katika mkutano mkuu wa SPC,2017 uliofanyika katika ukumbi wa
Katemi Hotel Novemba 4,2017.Picha zote na Patrick Mabula na Frank Mshana
- Shinyanga Press Club
Mgeni rasmi wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) mwaka 2017,Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua
mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika mkutano
huo.Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga,Shaaban Alley na katibu mtendaji wa SPC,Stephen
Wang'anyi wakimsikiliza mkuu huyo wa wilaya.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde akitoa hotuba fupi wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC)
mwaka 2017.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kulia
ni Katibu Msaidizi wa SPC,Ali Lityawi
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde akiwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi
wa habari na kutoogopa kufichua maovu yanayofanyika katika jamii
Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Katibu Mtendaji wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Stephen Wang'anyi akisoma taarifa ya mafanikio ya klabu hiyo tangu mwaka
2015 mpaka Oktoba 31,2017
Wanachama wa SPC,Kareny Masasy na Marco Mipawa (kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri ukumbini
Wanachama wa SPC wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde akitoa neno wakati wa majadiliano ya ajenda mbalimbali wakati wa
mkutano huo.Kulia ni Mweka Hazina wa SPC,Stella Ibengwe.
Picha ya pamoja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na
wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) wakati
wa mkutano mkuu wa SPC 2017
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya SPC
Picha ya pamoja, mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
(katikati),Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga,Kadama Malunde (kulia) na Katibu Mtendaji wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi
Picha zote na Patrick Mabula na Frank Mshana - Shinyanga Press Club
0 comments:
Post a Comment