KIJANA
mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kijiji cha Isagala, wilayani Kishapu,
mkoani Shinyanga, ameuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi
wakimtuhumu kuiba kuku wanne.
Aidha
katika tukio la wilayani Tarime mkoani Mara, mtuhumiwa wa ujambazi wa
kutumia silaha , Senso Mwita ameuawa katika kile kilichoelezwa ni kwenye
majibizano ya kurushiana risasi na polisi.
Kuhusu
anayetuhumiwa kuiba kuku, Polisi imemtaja ni Ngaga Shija ambaye alipewa
kipigo na kisha mwili wake kuchomwa moto, alikuwa akituhumiwa kuiba
kuku hao katika kijiji cha Ikonda.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evaresti Mangala,
kabla ya kifo, Shija alikuwa nje kwa dhamana katika kesi iliyokuwa
ikisikilizwa Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, akikabiliwa na mashitaka
ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupatikana na mali ya wizi.
Aliuawa
juzi saa 2 asubuhi katika Kijiji cha Isagala Kata ya Mwamashele
wilayani Kishapu. Hata hivyo Kamanda alisema mmiliki wa kuku wanaodaiwa
kuibwa, hajafahamika.
Katika
tukio la wilayani Tarime, mkoani Mara, mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia
silaha , inadaiwa alikuwa na wenzake wawili ambao walijibizana na
polisi kwa kurushiana risasi.
Mwita
anayekadiriwa na umri wa miaka kati ya 25 na 30, inadaiwa alikuwa
akisakwa na Polisi muda mrefu kwa kuhusika na matukio ya unyang’anyi wa
kutumia silaha na mauaji katika Tarafa ya Ingwe.
Kamanda
wa Polisi Tarime / Rorya, Justus Kamugisha alisema mwezi uliopita
kulikuwa na matukio ya mauaji ya watu katika vijiji vya Keisangura ,
Nyamwaga , Genkuru, Mriba na Nyarero.
Alisema
usiku wa kuamkia Januari 5, Polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema
juu ya kuwepo na kuonekana kundi la majambazi katika kitongoji cha
Ntarechagini Kijiji cha Nyamwaga.
“Wakati
askari wetu wakiwa njiani kuelekea katika kitongoji hicho, ghafla
walishambuliwa kwa kurushiwa risasi na majambazi watatu na hapo ndipo
askari wetu walianza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmoja wao kwa
jina la Senso Magabe Mwita,” alisema Kamanda.
Kwa
mujibu wa Kamanda, Mwita alikuwa na silaha aina ya SMG iliyofutwa namba
zake na risasi 21. Wenzake walitoroka na yeye alifariki kutokana na
majeraha ya risasi akiwa njiani kupelekwa hospitali ya wilaya.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment