Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
Martin
alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya
kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya
kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin
alisema, "Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu
tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea
wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii
inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu"
"Vijana
wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu
wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu
lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo
uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira"
aliongezea Martin.
Aidha,
Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni
kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini
ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya
na Amerika.
Mmari
aliongezea, "Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali,
usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga
nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi
chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa
kwenye programu"
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga
wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na
vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa
upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo wameshukuru kwa
nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo
tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.
Mmoja
wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha, alisema kuwa
anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama
kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia
programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia
kutatua matatizo hayo.
"Nimekuwa
sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona
nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania" aliongezea Bi. Malamsha.
Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
|
Naye
kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua
programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha
biashara.
"Nimeweza
kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika
na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya
kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe" alimalizia Said.
Raleigh
Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani
Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo la kuisaidia jamii
ya Tanzania sehemu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment