Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo akiagana na Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -
SPC) ,Kadama Malunde (kushoto) - Picha na Shinyanga Press Club.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo akizungumza na waandishi
wa habari mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Julai 21,2017 katika ukumbi wa
jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club
- SPC) ,Kadama Malunde akizungumza wakati Kamanda Muliro akiagana na
waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo akiagana na Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -
SPC) ,Kadama Malunde.
Katikati
ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
(Shinyanga Press Club - SPC) ,Shaaban Alley akifurahia jambo na Kamanda
Muliro.
Wa
kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa
wa Shinyanga (SPC) , Stephen Wang'anyi,akifuatiwa na Mwenyekiti wa
SPC,Kadama Malunde,kamanda Murilo na Makamu Mwenyekiti wa SPC ,Shaaban
Alley wakiwa katika picha ya kumbukumbu.
Waandishi wa habari mjini Shinyanga wakiwa katika picha ya kumbukumbu na kamanda Muliro.
Waandishi
wa habari waliopo mjini Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na
kamanda Muliro. Hawa ni miongoni mwa waandishi wa habari 91 waliopo
mkoani Shinyanga ambapo kati yao zaidi ya 50 wapo mjini Kahama.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliopo mjini Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na kamanda Muliro.
Picha zote na Shinyanga Press Club
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo aliyekuwa kamanda Polisi
Mkoa wa Shinyanga kuanzia Mwezi Agosti mwaka 2016 hadi mwezi Julai
mwaka huu, leo Ijumaa Julai 21,2017 ameagana na Waandishi wa habari mkoa
wa Shinyanga tayari kuanza kutekeleza majukumu yake ya Ukamanda wa
polisi katika mkoa wa Kinondoni.
Julai
18,2017, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro alifanya
mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.
Kufuatia
mabadiliko hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo
cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake imechukuliwa na
Kamanda Muliro huku nafasi ya Muliro ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi
wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa
Polisi wa Mkoa wa Mara.
Akizungumza
leo wakati wa kuagana na waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga,
Kamanda Muliro aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga pamoja na
waandishi habari kwa ushirikiano waliokuwa wanampatia tangu afike mkoani
humo.
“Mwezi
Agosti mwaka 2016,nilipoteuliwa kuwa kamanda wa polili mkoa wa
Shinyanga,kitu cha kwanza nilichokifanya nilikutana nanyi na kuwaomba
ushirikiano wenu wa dhati katika utekelezaji wa majukumu yangu,nimeona
niwashukuru kwa dhati,nawashukuru wadau wote wa masuala ya kiusalama
katika mkoa wa Shinyanga,viongozi wa idara mbalimbali za
serikali,wananchi pamoja na wanahabari ambao kwa kiwango kikubwa
walinisaidia katika kutekeleza majukumu yangu”,alieleza Kamanda Muliro.
“Waandishi
wa habari nawapa nafasi ya pekee kwa sababu tangu mwanzo niliwaeleza
kuwa ili tuweze kutekeleza majukumu yetu ya masuala yanayohusiana na
haki ninyi mna nafasi kubwa,niliwakumbusha kuwa ninyi mna nafasi ya
kuona mbali wakati mwingine kuliko tunapoona sisi,mnapata habari
mbalimbali ambazo zilikuwa zinatusaidia sana kufanya uchunguzi na
kufanikisha kutoa haki kwa wananchi”,alisema Kamanda Muliro.
“Wote
mnakumbuka changamoto tulizokuwa nazo mkoani hapa,ikiwemo za wazee
kuuawa,unyang’anyi wa kutumia silaha,utekaji magari,ajali za
barabarani,makosa ya ndoa za utotoni,watu kujichukulia sheria mkononi
kwa kupitia ninyi mmenisaidia sana,tulipambana wote kwa pamoja na kwa
kiasi kikubwa tukafanikiwa na kuufikisha mkoa hapa tulipofika”,alisema Kamanda Muliro.
“Nimewaiteni
hapa ili kuwapa taarifa rasmi kuwa sasa naenda kutumikia mkoa wa
Kinondoni,naomba kamanda anayekuja mmpatie ushirikiano mlionipa,muwe
wawazi,watulivu,wavumilivu na jambo lolote mnaloona au kulisikia muweze
kulifanyia uchunguzi na wakati mwingine mpate habari upande wa pili kama
vile taaluma zenu zinavyoelekeza”,aliongeza Kamanda Muliro.
Akizungumza
kwa niaba ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde alimshukuru kamanda Muliro kwa
ushirikiano wote aliokuwa akitoa kwa waandishi wa habari kwa muda
muafaka pale walipohitaji ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ili
kuihabarisha na kuielimisha jamii ili kufichua na kutokomeza vitendo
vya kihalifu mkoani humo.
“Kamanda
Muliro hakuwa na tabia ya kupuuzia mambo anayoelezwa,alikuwa msikivu
siku zote amekuwa akitumia kauli ya “Jifunze Kusikiliza”,na mara kwa
mara amekuwa akifika katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga siyo tu kikazi bali hata kubadilishana tu mawazo”,aliongeza Malunde.
0 comments:
Post a Comment