WATU wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la Nkondo
lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza baada ya kugonga kichwa cha
treni eneo la Karogho Relini katika Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule
alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa tatu usiku juzi barabara kuu
iendayo Maganzo wakati basi hilo lenye namba za usajiri T 693 BUW aina
ya Youtong mali ya Kampuni ya Nkondo likiendeshwa na dereva Emmanuel
Warengo (34).
Kamanda alisema katika ajali hiyo, watu wawili Ramadhani Juma (38) na
Eva Brown (29) walijeruhiwa kwa kuumia kifuani na kukimbizwa Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa kwa kupata matibabu. Alisema chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa dereva wa basi kutochukua tahadhari wakati wa kuvuka barabara
katika njia ya treni na alikimbia baada ya ajali hiyo na Polisi
wanaendelea kumtafuta.
Katika matukio mengine, Polisi imefanya oparesheni na kuwakamata
watuhumiwa 29 wa makosa mbalimbali, kati ya hao saba kwa tukio la
ukataji panga kikongwe mmoja aliyepo wilayani Kishapu. Kamanda alisema
katika oparesheni hiyo walikamata pikipiki saba, mifuko ya saruji 14,
magodoro mawili, vifaa vya kupigia ramli chonganishi, vifaa vya kufanyia
uhalifu, difu 15 za matolori, mabomba 14 ya kutengenezea pombe aina ya
gongo, mashine za kuvutia maji mbili na ya kuchomelea moja.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment